Msanii wa bongo flava Boniventure Kabogo – Stamina (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote mjini Morogoro leo. Tigo imetangaza punguzo la bei kwa tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR pamoja na kuzindua shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo. Pamoja naye ni (kuanzia kushoto), Mtangazaji wa kituo cha Clouds FM Gardner Habash, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Morogoro, Stephen Kunambi, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo – William Mpinga, Afisa Michezo wa Manispaa ya Morogoro - Asteria Mwang’ombe , msanii wa bongo flava Abednego Daniel – Belle 9, na mtangazaji wa Clouds FM Kenneth Frank – Kennedy the Remedy.
Wasanii wa Bongo Flava (kuanzia kushoto) Z Anto, Mr Blue Kabayser na Ben Pol wakisalimiana wakati wa hafla ya uzinduzi wa uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote mjini Morogoro leo. Tigo imetangaza punguzo la bei kwa tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR pamoja na kuzindua shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo. Tamasha la kwanza la msimu huu wa Tigo Fiesta 2018l inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro siku ya Jumamosi.
---
Huku nchi nzima ikisubiri kwa hamu kuanza kwa msimu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote, mdhamini mkuu Tigo Tanzania pamoja na waandaaji Clouds Media Group wameanza maandalizi rasmi ya tamasha hilo litakalorindima Jumamosi hii tarehe 29 Septemba katika viwanja vya Jamhuri, mjini Morogoro..
Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 – Viba Kama Lote, Gardner G. Habash aliwahakikishia wote watakaohudhuria tamasha hilo usalama na mapokezi mazuri. ‘Tunawakaribisha nyote kwenye shamrashamra za mwanzo wa msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote,’ Gardner alisema.
‘Tigo inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Morogoro, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim,’ Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema. Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.
‘Katika miaka ya hivi karibuni, tumetambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotokana na tamasha la Tigo Fiesta. Bali na kutoa fursa ya kuutangaza mkoa husika, pia inaongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama nitilie, vyombo vya usafiri kama vile bodaboda, kumbi za starehe na biashara nyinginezo,’ Gardner aliongeza.
Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu litashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments: