Kwa miaka mingi TGNP Mtandao imekuwa ni tanuru la kuwapika wanawake vijana pamoja na watoto kuweza kupambana na kutete haki zao kwa njia zilizokuwa salama na zenye kukubalika kikatiba.
Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao, Anna Sangai akitoa ufafanuzi wa jambo katika semina ya maandalizi ya miaka 25 ya shirika hilo iliyofanyika makao makuu ya shirika hilo Mabibo jijini Dar es salaam.
Hayo yameelezwa na Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Anna Sangai alipokuwa akiendesha semina ya jinsia na maendeleo mapema wiki hii makuu ya shirika hilo yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam.
Akiongea katika semina hiyo afisa huyo alisema kuwa TGNP Mtandao inatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake, na maadhimisho hayo yatakuwa yamekusanya wadau mbalimbali wakiwemo washirika walioweza kushiriki kwa namna moja au nyingine katika miaka hiyo yote.
Lakini pia maadhimisho hayo yatawafanya kukaa pamoja na wadau wake kujitathmini katika mambo mbalimbali ikiwemo changamoto na kujipongeza katika maswala mengi waliofanikiwa kuyatekeleza au kuyapigania yakaingia katika sera na mipango ya serikali ama sekta binafsi ambayo yataweza kuisaidia jamii.
Mwanaharakati na Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Makumbusho Janeth Mawinza akitoa mchango wake katika semina ya maandalizi ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya TGNP Mtandao.
Aliendelea kusema kuwa TGNP imekuwa ni chachu ya maendeleo kwa jamii lakini pia kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika mikutano ya uibuaji, kupigania bajeti yenye mlengo wa kijinsia pamoja na upatikanaji wa huduma za kijamii kama Elimu, Maji, Umeme, huduma za afya nk.
Afisa huyo alisisitiza kuwa TGNP imeendelea kuwa ni mtetezi wa haki za wanawake na watoto kwa kupinga mambo mbalimbali ya ukatili wa kijinsia katika jamii, hivyo basi watayachukua mambo hayo na kuyaweka kwa pamoja kwa mfumo wa matukio na kuweza kuwashirikisha watu wengine kuona kilichofanyika ndani ya miaka hiyo yote 25.
Akiongelea baadhi ya mafanikio yaliyoweza kupatikana kwa miaka hiyo 25 ni pamoja na bajeti yenye mlengo wa kijinsia japo kuwa haijaweza kufikiwa kwa kiwango sahihi lakini kuna matumaini makubwa yakufiki na jambo lingine ni kuondolewa kodi kwa taulo za kujihifadhia watoto wakike pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mengi uliohusisha hasa wanawake.
Wananchi kutoka kata mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakifuatilia semina.
Toa Maoni Yako:
0 comments: