Baadhi ya Viongozi wakiwa katika eneo la Pugu Bangulo jijini Dar es Salaam leo walipotembelea kutatua mgogoro wa ardhi uliokuwa ukitokea katika eneo hilo la Pugu Bangulo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Pugu Bangulo jijini Dar es Salaam leo.
Wananchi wa Pugu Bangulo wakiwasikiliza viongozi mbalimbali waliofika kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo la Pugu Bangulo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wa Pugu Bangulo wakiwasilikiliza viongozi waliofika leo katika eneo lenye mgogoro.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kwa pamoja wamemaliza mgogoro uliodumu kwa muda mrefu katika eneo la Pugu Stesheni na Bangulo na kuwakabidhi eneo la hekari 1792 walilokuwa wamevamia.

Akitoa maamuzi hayo Waziri mwenye dhamana ya mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina mbele ya wananchi hao amesema kuwa amekubali kuwapa eneo hilo na huku akiwataka wananchi hao kutovamia hekari 108 zilizobaki kwani zitaendelea kuwa za serikali.

Hayo ameyasema Mpina hapa katika eneo la pugu mnadani ambapo mkutano mkuu wa kuwakabidhi ulifanyika hatua iliyoibua vifijo na vigeregere kutoka kwa wananchi hao.

"Nasema nimekubari kuwapa eneo hili la hekari ,1792 lakini nawaomba hekari 108 zilizobaki wasizivamie tena na yeyote atakayefanya hivyo hatavumiliwa kamwe na atakuwa ameingia kwenye mgogoro mkubwa na serikali."alisema Mpina.

Mpina amesema maamuzi hayo yamelenga kwenye maeneo ya Pugu station na Bangulo si kinyume na hapo nakwamba katika eneo lililobaki halitoi fursa ya kuendelea kuwa na mnada katika eneo hilo na badala yake watahamisha mnada huo nakupeleka mahala kungineko.

Pia baada ya kutoa maamuzi hayo Luhaga mpina aliwataka wananchi hao kuendelea kuishi kwa amani na upendo na kuheshimu na eneo lililobaki litapimwa na kubadilisha matumizi nakuwaeleza wananchi hao kuwa wanasalimiwa na Rais Dkt John Magufuli.

Kwaupande wake Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza katika mkutano huo alisema wao kimsingi wamekubarianan na hilo na watakachofanya nikuangalia eneo lingine la kuepeleka mnada huo.

Amesema kuwa baada ya kuwapa eneo hilo hatua inayofuata nikubadilisha hati kutoka kwenye miliki ya Serikali na kutoa kwa wananchi hao.

"Nasema kuwa hatua Inayofuata ni wanachi hao kutengeneza kamati ambayo itashughulikia upatikanaji wa hati miliki na kuweza kurasmishwa rasmi."alisema Lukuvi

Lukuvi alisema wao kama serikali baada ya wananchi hao kukamilisha taratibu zote watakuja kupanga miundombinu yake ikiwamo kuweka mitaa,maji,na mambo mengine .

Kwaupande wake mkuu wa mkoa Dar es Salaam Paul Makonda aliwapongeza mawaziri hao huku akisema sasa anajisikia vizuri nathamani ya kuwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama inakuwepo.

Amesema wamefanya kazi kubwa na kinachoendelea nikutatua changamoto hizo za migogoro ya ardhi katika maeneo.mengine katika jiji la Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: