Mabondia Bushiri Kulwa na Seba, watakaopambana kuwania ubingwa wa Dunia katika uzito wa Cruiser.
Picha nyingine ni mabondi watakaopanda ulingoni mataji mbalimbali katika uzito wa Welter weigths'
Mratibu wa mpambano huo Shomari Kimbau akizungumza na wanahabari(hawapo pichani) katika moja ya mapambano yake.
MABONDIA 18 leo wanatarajia kupanda ulingoni katika ‘Uringo’ wa CCM Mwinjuma uliopo Mwananyamala kuwania mataji mbalimbali katika mchezo wa ngumi likiongozwa na pambano la raundi kumi kati ya Bushiri Kulwa na Seba.
Mapambano hyao yaliyoandaliwa na Kampuni ya ‘Golden Boy Africa’ yanawakutaniosha mabondia hao wanaowania mkanda wa Dunia katika uzito wa Kilo 84 ‘Cruiser weights’ linatajwa kuwa la kipekee na hasa kutokanana na viwango walivyonavyo mabondia wote wawili katika medani ya ‘masumbwi’
Mbali na pambano hilo ,.michezo mingine inatarajiwa kuwakutanisha mabondia Simba na Allen, Chidi Mbishi dhidi ya Moro Best,Mkalekwa Junior dhidi ya Abdala Luwanje, Hamisi Maya dhidi ya Karage Suba itakayochezwa kwa raundi nane kila mmoja.
Mapambano mengine ambayo ni pamoja na bondia Mbunju Laga dhidi ya Iman Tavez, Nurdin Mohammed dhidi ya Issa Mbwana , Mlekwa dhidi ya Rama, pamoja na pambano kati ya Modest John dhidi ya Kassim Juma, yote yakichezwa kwa raundi 6.
Mratibu wa mapambano hayo Shomari Kimbau, alisema tayari maandalizi yote yamekwisha fanyika ikiwemo mabondia kupima afya zao kabla ya mchezo na kwamba kinachosubiriwa na kutimia kwa muda husika.
Alisema ‘mpambano’ huo unaotarajiwa kuanza saa 10 za jioni, unatarajiwa kuwa wa kuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mabondia wote, hasa kutokana na namna ambavyo kila kambi ya mabondia hao iolivyojipanga ili kupata ushindi.
Awataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia vipaji kutoka kwa mabondia mbalimbali wa hapa nchinim huku akisisitiza uwepo wa suala la ulinzi na usalama kwa mashabiki watakaojitokeza kutazama pambano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: