Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale baada ya kuzindua rasmi Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam Septemba 27, 2018.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale (kulia) na Meneja Mkuu wa Kampuni ya SUMITOMO MITSUI, Bw. Ichiro Aok kutoka Japan wakiweka saini Mkataba wa kuanza ujenzi wa barabara ya juu (flyover) katika eneo la TAZARA.
---
Patrick Aron Nipilima Mfugale Alizaliwa katika eneo la Ifunda huko Iringa.

-Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa

-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.

-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi

-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India

-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.

-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.

-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, Braunshweig nchini Uingereza

-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.

-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.

-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System

-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.

-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .

Alibuni daraja la Magarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.

-Baadhi ya madaraja alioweza kujenga ni:

Daraja la Mkapa RufijiDaraja la Umoja linalounganisha tanzania na Moxzambique huko Ruvuma.Daraja la Rusumo huko MaraDaraja la Kikwete huko Magarasi.Daraja la Nyerere huko Kigamboni

- Mfugale ambaye kwa sasa ni mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.

Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.

- Ni Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.

- Ni mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.

-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: