Toleo la gesi asilia likiwa limeshafungwa baada ya kukamilika kwa kazi ya utoboaji wa bomba hilo
Wataalam wakiandaa Mtambo wa kutoboa bomba la gesi asilia ili kuruhusu kujenga toleo la gesi asilia.
Wajenzi wa Toleo wakiwa katika hatua za mwisho za kuweka Pig Coupon kifaa kinachowezesha kifaa cha usafishaji wa bomba kupita ndani ya bomba bila kukwama kwenye toleo hilo
---
Uwepo wa bomba la gesi asilia nchini umekua ni kivutio kikubwa cha uwekezaji wa viwanda haswa katika maeneo ambayo bomba hilo limepita jambo ambalo linafanya ndoto za Tanzania ya viwanda kutimia.
Meneja Mkuu wa GASCO Mha. Baltazar Mrosso ameeleza haya mara baada ya kukamilika kwa kazi ya utoboaji wa bomba la gesi asilia na kuweka toleo katika kijiji cha Mwanambaya Wilayani Mkuranga kwa ajili ya kuwasambazia wateja wa viwandani katika Wilaya hiyo.
“Leo hii tumekamlisha kwa mafanikio kutoboa na kujenga toleo katika eneo hili Mwanambaya kwanza ni ushindi kwetu kwakuwa tumeweza kutenganza kitivo kingine cha kuvutia uwekezaji wa viwanda katika eneo hili ambalo ni eneo la viwanda, pili kwa kujenga toleo hili ni heshima kubwa kwetu kama Shirika kuweza kuendelea kuunga mkono juhudi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya viwanda, pia kuhakikisha kazi hii inafanyika bila kuathiri utendaji wa kawaida wa bomba la gesi asilia ili wateja wetu wanaotumia gesi asilia sasa hivi waendelee kutumia gesi asilia katika viwada vyao ni mafanikio makubwa kwetu” alifafanua Mha. Mrosso.
Akielezea teknolojia ya utoboaji wa bomba la gesi asilia bila kufunga gesi inayopita ‘hot tapping’ Mha. Mrosso aliweka wazi kuwa hii ni mara ya kwanza toka shughuli za ujenzi wa mabomba zianze takriban zaidi ya miaka 10 na kwamba imetupa uhakika kwetu sisi kama Shirika kuweza kuwapatia wateja gesi asilia popote pale penye bomba lakini pia kuhakikisha uwekezaji wa viwanda unawezekana mahali popote penye bomba la gesi aslia na hivyo kuifanya mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Dar es Salaam kuwa vivutio vya uwekezaji kutokana na uwepo wa nishati bora na ya uhakika.
kujenga toleo sehemu ambayo haikuweka toleo kwa ku Uwwepo wa teknoloji ya kutoboa bomba la gesi asilia popote pale na kuweka matoleo ya kusambaza gesi asilia kwa wateja ni ushindi mkubwa wa kuhakikisha popote penye bomba la gesi asilia viwanda vinaweza kujengwa na sisi kama wasimamizi na waendeshaji wa bomba hilo tutawajibika kwa heshima zote kuhakikisha wateja wanapatiwa gesi asilia bila vizingiti vyovyote”
Mha. Mrosso amesema kuwa uwepo wa bomba la gesi asilia linalotoka Mtwara katika mikoa yote linapopita yaani Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam linafungua fursa ya upatikanaji wa nishati ya gesi asilia ya kutosha, bei nafuu na kwa uhakika katika kila sehemu lilipopita na hivyo kufanya uwekezaji wa wa viwanda kuwa rahisi Zaidi na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa viwanda.
Akiongelea hali ilivyo kwa sasa ya upatikanaji wa nishati haswa kwa matumizi ya viwanda, ndugu Mrosso ameeleza kuwa, kumemkuwepo na unafuu mkubwa kwa sasa zaidi ya hapo awali kabla ya gesi asilia kuanza kuzalishwa kwa wingi na kutumika viwandani ambapo muwekezaji alialazimika kununua mafuta mazito au dizeli ili kuweza kuendsha mitambo mbalimbali ikiwemo majenereta na hivyo kufanya sekta ya viwanda kudorora hali ambayo imebadilika kwa kiasi kikubwa baada ya viwanda kuanza kutumia gesi asilia.
“Gesi asilia na nafuu Zaidi kuliko mafuta ambayo ndiyo yamekuwa yakitumika kwa wingi kuendeshea mitambo mbambali viwandani hii kutokana na punguzo kubwa la bei gesi asilia kwa ambayo tunawauzia wateja wetu ambao tayari wamekuwa wanatumia gesi asilia kuendesha mitambo mbalimbali kwenye viwandani vyao ambapo wamekuwa wakiokoa zaidi ya asilimia 30 ya gharama za nishati na uendeshaji.
“TPDC kupitia kampuni yake tanzu ya GASCO inafanya kila linalowezekana kuhakikisha upatikanaji wa gesi asilia unakua mkubwa kwa kujenga miundombinu ya kuweza kusambaza gesi hiyo kwa wateja wa sasa na wa baadae ili kufaniskisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuleta mageuzi ya uchumi wa viwanda nchini kwa kuviwezesha viwanda kufikia viwango bora vya ufanisi wa uzalishaji wa bidhaa, kuweza kutumia gharama ndogo za uzalishaji wa bidhaa ili kufikia ubora utakaomudu ushindani wa soko la bidhaa ndani na nje ya nchi” amefafanua Kaimu Meneja Mkuu wa GASCO.
Toa Maoni Yako:
0 comments: