Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akiongea wakati wa uzinduzi wa Siku ya Kimataifa ya Wazee leo jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Bw. Fabian Daqaro akiongea wakati wa ufunguzi wa uzinduzi wa Siku ya Kimataifa ya Wazee leo jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha wakwanza kushoto Bw. Fabian Daqaro, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu katikati na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Naftali Ng’ondi wakikagua baadhai ya kazi za ujasiliamali za kikundi cha wazee walipotembelea mabanda ya Wazee kujionea shughuli zao.
Wazee wa Jiji la Arusha walijitokeza kwa wingi kupima Afya wakati wa madhimisho ya Siku ya kimataifa ya Wazee yanayoendelea Jijini Arusha.
Wazee wa Jiji la Arusha walijitokeza kwa wingi kupima Afya wakati wa madhimisho ya Siku ya kimataifa ya Wazee yanayoendelea Jijini Arusha.

Wazee 576,370 wamenufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini nchini tangu februari mwaka 2018 chini ya TASAF na kati ya hao wanaume ni 217,947 na Wanawake 358,423 kwa pande zote za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema hayo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee leo mjini Arusha akitaja Siku hii kuwa inatukumbusha wajibu wetu katika kuwalinda, kuwatetea na upatikanaji wa huduma bora kwa wazee.

Aidha Dkt. Jingu ameongeza kuwa serikali inatekeleza Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 kwa kuanzisha Mpango wa Utambuzi wa Wazee katika Halmashauri na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila malipo wazee wote wasiojiweza hapa Nchini.

Aidha pamoja na utekelezaji Sera hiyo pia aserikali inaandaa Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza mauaji ya wazee ambao utazinduliwa ifikapo Juni mwaka 2019 lakini pia serikali itapitia Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 ili iendane na hali halisi ya maisha ya Wazee.

‘’Kutokana na umuhimu wa uwepo wa wazee katika familia, jamii na Taifa letu hatuna budi kuitumia siku hii ya leo kuhamasishana, kuelimishina na kukumbushana wajibu wetu kwa wazee wetu ili kuwawezesha kuishi maisha bora yenye staha’’. Aliongeza Dkt. John Jingu.Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Fabian Daqaro ambaye amezindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee ya Mwaka 2018 amesema wazee wote watanufaika na msamaha wa kodi wa nyumba ambazo wanaishi lakini msamaha huo hautausika na nyumba zote za biashara kama vile vyumba vya maduka au nyumba za kupangisha.

‘’Naomba nieleweke vizuri kama nyumba yako ni kuishi na haitumiki kwa biashara itapata msamaha wa kodi lakini kama nyumba yako au nje ya nyumba yako yenye uzio ina sehemu za kufanyia biashara itatozwa kodi ya serikali nendeni ofisi za Mapato nakuweka takwimu zenu sahihi watawahudumia’’.Alisistiza Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Fabian Daqaro.Mkuu huyo wa Wilaya Arusha pia amewataka watendaji wa Idara ya Afya Mkoani humo kuweka kumbukumbu sahihi za Wazee mkoani humo ili wazee waendelee kutambuliwa ili kuwawezesha wazee hao kupata huduma muhimu ikiwemo Afya,malazi chakuala, ulinzi na hifadhi ya Jamii ya Uzeeni.

Siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani huadhimishwa hapa Nchini kila tarehe 1 mwezi wa kumi kufuatia Azimio la Umoja wa Mataifa linalozitaka Nchi Wanachama kutenga Siku maalumu ya kutafakari mchango wa wazee katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: