Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
BARAZA la sanaa la Taifa limetoa ufafanuzi wa kanuni za baraza hilo zitakazokuwa zinatumika kuendeshea kazi za sana hapa nchini.
Kanuni hizo zilizoanza utekelezaji wake mwaka huu katika kusimamia shughuli zote zinazohusiana na sanaa.
Akifafanua kanuni hizo Afisa Sanaa wa Basata Augustino Makame leo katika ofisi zao Jijini Dar ea Salaam amesema kuwa baadhi ya sehemu za kanuni hizo zimebainishwa.
Ambazo ni muundo wa baraza, usajili na vibali vya kazi,uwasilishwaji wa taarifa kwa msajili,kufutwa kwa usajili,masharti ya jumla kwa wadau wa kazi za sanaa,masharti ya jumla ya kazi za sanaa,makosa na adhabu,uzingatiaji wa sheria katika kazi za sanaa.
Afisa huyo amesema baraza ndilo litakalokuwa msajili mkuu na mtoa vibali vyote vya kufanya kazi za sanaa kwa wasajili.
"Msajili atatoa kibali na kitambulisho cha kufanya kazi za sanaa kwa mtu au kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa kanuni hizo, amesema makame"
Aidha Makame amesema mtu yoyote hatoruhusiwa kufanya kazi za sanaa bila kusajiliwa na baraza au upelekwa sokoni ama kwa walaji kabla ya kupewa kibali cha kuthibitishwa kuwa na maudhui na madili kuzingatiwa, ambapo kibali kitalipwa kila mwaka kwa mujibu wa ada zitazolipwa katika halmashauri husika.
Vile vile amesema shughuli zote zinazohusiana na sana zitafanyika kwa kuzingatia sheria zote za jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kanuni zake.
Makame amemalizia kwa kusema kuwa endapo kazi ya msajili yeyote itakiuka masharti ya kanuni hizo msajili huyo atachukuliwa hatua na baraza kwa mujibu wa kanuni 64 (1) au (2), itakuwa ni kosa la jinai na kwa mtandao wowote ama chombo chochote cha habari kurusha kazi hiyo kwa namna yoyote ile.
Toa Maoni Yako:
0 comments: