Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisamiliana na baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) wakati alipowatembelea jana kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wa kanda ya Kusini, Ebramtino Mgiye mara baada ya kuwasili jana kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) wakati alipowatembelea jana kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga(katikakati) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii. (PICHA ZOTE ZA LUSUNGU HELELA-MNRT).

Watumishi wa Wakala wa Huduma Tanzania (TFS) wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria za utumishi wa Umma ili kuleta ufanisi wakati wanapotekeleza majukumu yao ya uhifadhi.

Rai hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati alipowatembelea jana watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii

Amewataka kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu na yeyote atakayetuhumiwa kupokea rushwa hata kama hajapokea rushwa hiyo kutoka wafugaji kwa makubaliano ya kuingiza mifugo hifadhini kwa makubaliano ya malipo atashughulikiwa ipasavyo.

Aliongeza kuwa endapo watumishi hao wataweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo hakuna kiongozi yeyote watakayesumbuana nao

‘’Tunataka mfanye kazi zenu za uhifadhi kwa weledi wa hali ya juu na mkifanya vizuri basi nakuwa nimefanya mimi na mkifanya vibaya mnakuwa mnaniangusha mimi hivyo sitokubali’’ alisisitiza Naibu Waziri Hasunga.

Aidha, Amewata wafanye kazi kwa kushirikiana na jamii kwa vile hakuna shughuli yeyote itakayofanikiwa endapo wananchi wataachwa nyuma.

‘’Tunataka jamii ione faida ya moja kwa moja kwa kupata elimu kuhusu uhifadhi pamoja na kushirikishwa kwenye masuala yote ya misitu ili waweze kutoa ushirikiano wakati ukataji miti unapofanyika popote pale’’

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo amewataka watumishi hao kuchukua likizo kila mwaka na kuitumia likizo hiyo kwenda sehemu mpya kutalii na kupumzisha akili na kujifunza vitu vipya baadala ya kila likizo kwenda kijiji walikozaliwa kama ilivyozoeleka kwa watumishi wengi.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu, Kanda ya Kusini, Ebramtino Mgiye alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa licha ya kuwa na changamoto ya uhaba wa vitendea kazi lakini kila mtumishi kwa nafasi yake amekuwa akitimiza wajibu wake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: