Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu akihoji matumizi ya fedha zinazokusanywa katika maeneo mbalimbali katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi uliofanyika leo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mheshimiwa Ali Juma Mwanga, akiendesha mkutano huo wa madiwani.
Madiwani wakiwa kwenye baraza hilo kujadili mambo mbalimbali.
Diwani wa Kata ya Mtunduru, Ramadhani Mpaki akichangia jambo kwenye baraza hilo.
Wakuu wa idara mbalimbali wa Halmashauri hiyo wakifuatilia kikao hicho.
Waandishi wa kumbukumbu za vikao wakiwa pamoja na viongozi wa vyama vya kisiasa wakiwa katika mkutano huo.
Waandishi wa kumbukumbu za kikao hicho wakiwa kazini kuchukua taarifa mbalimbali.
Madiwani wakiwa katika kikao hicho.
Wakuu wa idara mbalimbali wa Halmashauri hiyo wakiwa katika mkutano huo.
Madiwani wakiwa kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Dumunyi, Mheshimiwa, Nkhangaa, akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Ntuntu, Omari Athumani Nkoki Toto, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ikungi, Rustika Turuka, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Na Robert Julius, Ikungi.
MBUNGE wa Jimbo la Uchaguzi la Singida Magharibi, Mhe Elibariki Kingu amehoji matumizi ya fedha zinazokusanywa kutoka maeneo mbalimbali ya Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi.
Kingu alihoji matumizi ya fedha hizo kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa wilaya hiyo uliofanyika mjini Ikungi leo hii..
"Napenda kujua matumizi ya fedha zinazo kusanywa katika halmshauri yetu" aliuliza Kingu.
Katika hatua nyingine Kingu aliuliza utaratibu utao tumiwa katika kukusanya mapato hayo kuwa unapaswa kufuata sheria na si vinginevyo.
Maswali mengi yaliyokuwa yanaulizwa na madiwani hao yali lenga kujua fedha zinazokusanywa na wananchi kwa ajili ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali kama zinawafikia walengwa ambao ni wananchi kwa ajili ya kutumika kwenye miradi.
Mbunge alihoji fedha za makusanyo katika wilaya ya Ikungi zinakwenda wapi katika kikao kilichofanyika katika mkutano wa madiwani wa Ikungi na kusema kama kuna watu wanakusanya fedha za wananchi pasipo utaratibu husika basi sheria ifuatwe ili kukabiliana na watu wa aina hiyo.
MMkutano huo uliongozwa na Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Ally Juma Mwanga na kufuatiwa na uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo na Kamati ya kudumu ya madiwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: