Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Manyara, Mhandisi Bashiri Rwesingisa akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (aliyevaa kofia) kuhusu hatua iliyofikia ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Mizani ya kudumu katika eneo la Mwada-Mbuyu wa Mjerumani, Wilayani Babati. Mkoani Manyara.
Muonekano wa eneo la Mwada Wilayani Babati itakapojengwa mizani na kituo cha pamoja cha ukaguzi wa magari mkoani Manyara.
Muonekano wa mto Manyara ambapo linajengwa daraja la Magara lenye urefu wa mita 84, wilayani Babati Mkoani Manyara. Daraja hilo linatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 24.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Manyara kuhusu kuzingatia viwango katika ukarabati wa barabara sehemu ya mlima Magara kwa kiwango cha zege mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Mkoani Manyara.
Mafundi wakindelea na ujenzi wa barabara sehemu ya Magara kwa kiwango cha zege, Mkoani Manyara.
Muonekano wa barabara Magara-Mbulu ambayo inafanyiwa ukarabati na Wakala wa Barabara Nchini (TNAROADS) kwa kiwango cha zege,Mkoani Manyara.
Toa Maoni Yako:
0 comments: