Dk.Hezron Kiwale Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mwananyamala akipokea Mashine mpya ya kufulia nguo na vifaa tiba mbalimbali vilivyotolewa na Benki ya Accsess kutoka kwa Sijaona Simon Afisa Masoko Mwandamizi wa benki hiyo katika hospitali hiyo leo, Vifaa tiba hivyo vina thamani ya shilingi milioni 3 za kitanzania.
Dk.Hezron Kiwale Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mwananyamala na Sijaona Simon Afisa Masoko Mwandamizi wa benki ya Accsess wakiangalia mashine ya kufulia iliyotolewa na Benki ya Accsess hospitalini hapo.
Sijaona Simon Afisa Masoko Mwandamizi wa benkiya Accsess akimkabidhi Sister Dolla Macha Muuguzi Kiongozi wa Chumba cha Upasuaji hospitali ya Mwananyamala moja ya mashuka yaliyotolewa na benki hiyo kwa hiyo kulia ni Dk.Hezron Kiwale Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mwananyamala.
Dk. Hezron Kiwale Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mwananyamala akishukuru benki ya Access baada ya kupokea msaada huo wengine ni wauguzi wa hospitali hiyo.
Benki ya Access imekabidhi vifaa tiba mbalimbali kwa hosiptali ya Rufaa ya Mwanayamala jijini DSM. Akikabidhi vifaa hivyo leo Afisa Mwandamizi kutoka kitengo cha Masoko wa Access Bank Ndugu Sijaona Simon Malosha alisema kuwa benki ya Access imeona jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya na hivyo kuamua kuiunga mkono kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali ambavyo vitakua msaada mkubwa kwa wagonjwa na hospitali nzima ya mwananyamala.
‘Huu ni mwendelezo wetu katika kuchangia na kurudisha faida kidogo tunayoipata kwa Jamii. Huko nyuma benki yetu ilijikita sana kusadia sekta ya Elimu kwa upande wa Teknolojia ya Habari , lakini leo tumeamua kubadili mtazamo na kuweza kufanya kitu kwa ajili ya sekta hii ya afya ambayo imekuwa na changamoto nyingi sana. Leo tumekabidhi vifaa tiba mbali mbali ikiwemo hii mashine ya kufulia ambayo inauwezo wa kubeba kilo 16 kwa wakati mmoja na vile vile inauwezo wa kufua na kukausha.
Ninaamini vifaa hivi vitakuwa msaada mkubwa sana kwa hospitali hii hasa upande wa chumba cha upasuaji maana kuna vifaa vingi ambavyo ni kwa ajili ya chumba cha upasuaji., Tulipokuja katika hospitali hii tulielezwa kwamba kwa sasa wamekuwa hawana mashine ya kufulia mashuka baada ya upasuaji na hivyo kulazimika kuyapeleka muhimbili ili kufuliwa jambo ambalo linachukua muda mrefu’’
Akizungumzia kuhusu gharama, Ndugu Simon alisema vifaa vyote kwa ujumla vinathamani zaidi ya shilingi milioni tatu na alivitaja vifaa hivyo kuwa ni stendi za matone 9, mashuka kwa ajili ya chumba cha upasuaji na mashine ya kufulia.
Akishukuru kwa niaba ya hospitali ya mwananyama kaimu mganga mfawidhi Dr. Hezron Kiwale alisema, nipende kuwashukuru sana AccessBank kwa msaada wao huu , vifaa hivi vitakuwa msaada mkubwa sana kwetu kwani kumekuwa na upungufu mkubwa wa vifaa vingi kama hospitali ya rufaa na hivi walivotupa leo AccessBank ni baadhi tu , bado tunatoa wito kwa taasisi nyingine na wadau mbalimbali wa afya kuweza kuunga jitihada za serikali yetu kuimarisha sekta ya afya kama benki ya Access ilivyofanya. Tumekuwa tukipokea ahadi nyingi kutoka kwa wadau mbalimbali lakini bila mafanikio niwashukuru tena uongoz wa AccessBank na niwaombe kuwa wasituchoke bado tuna uhitaji wa vifaa vingi’’.
Toa Maoni Yako:
0 comments: