Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo (katikati) wakati Waziri huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akimwelezea haki na wajibu wa mlipakodi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakati Waziri huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi ambaye pia ni Mratibu wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Honester Nduguru akimtambulisha Afisa wa TRA kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally (wa pili kulia) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Afisa Mwandamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Julius Caesar wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Kefa Mwambene akimkaribisha Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benedict Liwenga).
Toa Maoni Yako:
0 comments: