Dominick Timothy Head of Wholesale Banking akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa branch ya Dodoma.
 Moja wa wageni waalikwa akiuliza swali wakati wa hafla ya uzinduzi wa branch ya Dodoma.
 Brendansia Kileo Meneja Masoko wa UBA Tanzania akikaribisha wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa branch ya Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Tanzania Bw. Usman Isiaka akifafanua jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa branch ya Dodoma.
Branch Manager wa UBA Dodoma Branch Bw. Onesmo Mwansanga pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Tanzania Bw. Usman Isiaka wakisalimiana mteja wa UBA wakati wa hafla ya uzinduzi wa branch ya Dodoma.





Na Mwandishi wetu, Dodoma

BENKI ya ‘United Bank Of Africa’ ‘UBA’ imefungua tawi jipya Jijini Dodoma huku ikiahidi kuendeleza mikakati yake ya kushirikiana na Serikali katika kusukuma maendeleo ya nchi kupitia ukuzaji wa uchumi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tawi hilo mwishoni mwa wiki Mkurugenzi wa UBA Tanzania Usman Isiaka, alisema pamoja na mambo mengine uzinduzi wa tawi hilo jipya umelenga mpango wa benki hiyo katika kutoa huduma bora kwa wananchi kulingana na matakwa ya uendeshaji wa huduma za benki hapa nchini.

Alisema benki hiyo yenye matawi manne nchini likiwepo tawi hilo la Dodoma, tangu kuanzishwa kwake hapa nchini imekuwa ikitoa huduma mbalimbali za kifedha na zenye kuzingatia viwango bora kwa wateja wa aina zote yakiwemo makampuni, sekta binafsi pamoja vikundi mbalimbali vya wajasiriamali.

“Malengo yetu ni kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwahudumia wateja wa makundi mbalimbali kulingana na vigezo vyao, hatua tunayoamini kuwa mbali na mambo mengine pia itasaidia kukuza uchumi wa Taifa na maendeleo kwa ujumla wake” alisema Isihaka

Aidha Isihaka alisema katika kuwafikia wateja wa maeneo mbalimbali nchini, UBA pia imeweza kuunganisha nguvu zake kwa kuwa na uishirikiano na baadhi ya benki za hapa nchini, ikiwemo benki ya CRDB kwa ajili ya kuwafikia wateja waliopo maeneo mbalimbali nchini na kuwapa huduma zozote pale wanapozihitaji.

Alisema UBA inayotoa huduma zake katika nchi 20 za Bara la Afrika Marekani, Uingereza na Ufaransa, ina mtaji wa Dola za Marekani zaidi ya Bilioni 12, na hivyo kujidhatiti katika utoaji wake wa huduma katika nchi yoyote. 

Alisema malengo mengine ya benki hiyo nchini ni kuhakikisha inaongeza wateja wake huku ikiweka masharti nafuu ya riba katika mikopo inayoitoa, kwa lengo la kuwawezesha wananchi, vikundi mbalimbali pamoja na taasisi kupata fursa ya kufaidika na mikopo hiyo na kujiendeleza katika shughuli mbalimbali.

Kwa upande wake Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Brendansia Kileo, mbali na kuwataka wananchi kujitokeza na kunufahika na huduma zinazotolewa na benki hiyo, aliwashauri wananchi hususani wafanyabiashara wakubwa na wadogo kujiunga na benki hiyo ili kunufahika na huduma zake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: