Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa akiongea na Walimu (hawapo pichani) walioshiriki katika kikao kazi cha kuandaa kitabu cha Maadili na Miiko ya kazi ya ualimu. Kikao hicho kilifanyika Mwishoni mwa wiki mjini Morogoro chini ya ufadhili wa EQUIP – Tanzania.
Mwakilishi wa EQUIP - Tanzania, Bw. Erick Kilala akiongea na washiriki wa kikao kazi cha kuandaa kitabu cha maadili na miiko ya kazi ya ualimu kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mmoja wa Washiriki wa Kikao kazi akichambua baadhi ya nyaraka kwa lengo la kufanya maboresho katika kuandaa kitabu cha maadili na miiko ya kazi ya ualimu.
Mmoja wa Walimu walioshiriki kikao kazi akitoa dondoo za madhui yanayohitajika katika kitabu cha maadili na miiko ya kazi ya ualimu.
Washiriki wakiwa katika vikundi kwa ajili ya kujadiliana namna ya kuandaa kitabu cha Maadili na Miiko ya Kazi ya Ualimu.
Katibu wa Tume ya Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa (katikati kwa waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na walimu walioshiriki kiko cha kuandaa kitabu cha maadili na miiko ya kazi ya ualimu. Kushoto (kwa waliokaa) ni mwakilishi wa EQUIP –Tanzania, Bw. Erick Kilala na Kulia (waliokaa) ni Mkurugenzi wa Huduma Saidizi kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Moses Chitama.
Toa Maoni Yako:
0 comments: