Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, ACP ,Hamis Issah akizungumza na madereva katika kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi wakati akifungua rasmi mafunzo kwa madereva hao ikiwa ni njia mojawapo ya kuwakumbusha Sheria ya Barabarani pamoja na matumizi ya Alama mpya za barabarani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah akiwaonesha Madereva baadhi ya Alama mpya ambazo zimeanza kutumika katika maeneo mbalimbali ya barabara.
Madereva wa Magari ya Abiria yanayofanya safari zake ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wakati akizngumza nao katika kituo Kikuu cha Mabasi mjini Moshi.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ,ASP,Zauda Mohamed akimuonesha jambo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,ACP,Hamis Issah wakati alipokutana na madereva wa magari ya Abiria,Kulia ni Mkuu wa Operesheni wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,ACP,Costantine Maganga na kushoto ni Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Ins,Peter Mizambwa.
Dereva mstaafu wa Magari makubwa ,Apolonary Malya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: