Neema hiyo imefikiwa Gairo baada ya ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Kuandikwa kufanya ziara Wilaya ya Gairo tarehe 27/6/2018.

Kazi kubwa iliyofanywa na Mhe. Shabiby Mbunge wa Gairo kwa kuwasemea wananchi wake kuhusu hali ya mtandao wa barabara za Gairo zilizo chini ya Tanroads hatimaye zimezaa na Matokeo ChanyA+.

Sasa barabara ya Gairo Nongwe imetengewa pesa za kutosha na hivi tunavyoongea mkandarasi yupo kazini Kata ya Rubeho.

Baada ya kumaliza barabara ya Magufuli ambayo ipo mjini Gairo sasa barabara hiyo inapandishwa hadi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kiwango cha lami.

Aidha barabara hiyo itaunganishwa kutoka Ofisi za CCM Gairo (W) kupitia Kata ya Magoweko hadi barabara ya lami Gairo Morogoro/Dodoma.

Barabara ya Gairo Kilindi ambayo inaunganisha Wilaya ya Gairo Kilindi, Kiteto, Mvomero nk sasa kuhengwa kwa kiwango cha lami. Pia kupitia barabara hii usafiri kwenda Makao Makuu ya nchi Jiji la Dodoma unaendelea kufunguka. Madaraja korofi yote kuanzia kata ya Chakwale (mto kaburi), Italangwe na Iyogwe sasa itakuwa historia.

Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. JJPMagufuli kwa kuifanya Gairo kuwa Wilaya Imara kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Wakulima endeleeni kuchapa kazi sasa mambo ni moto motooo. Tunategemea ndani ya miaka miwili kujenga Stendi ya Kisasa eneo la Ukwamani.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Gairo.

#Gairo Maendeleo Fasta kwa Mwendo Mdundo

#Hapa Kazi Tu!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: