Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na Naibu wake anayeshughulikia masuala ya
Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde wakifuatilia uwasilishwaji
wa michango ya wabunge kuhusu bajeti ya Ofisi hiyo wakati wa Bunge la
Bajeti Dodoma Aprili 11, 2017.
Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) wakinukuu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa
kujadili na kuipitisha bajeti ya Ofisi hiyo wakati wa Bunge la Bajeti
linaloendelea Dodoma.
Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia michango ya wabunge
wakati wa kujadili na kuipitisha bajeti ya Ofisi hiyo katika Bunge
linaloendelea Dodoma, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu (Bunge na Waziri
Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi na anayemfuata ni Katibu Mkuu (Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi Bungeni tarehe 11 Aprili,
2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na Mbunge wa Chambani (CUF) Mhe.
Yusuf Salim nje ya Viwanja vya Bunge Dodoma wakati wa Bunge la Bajeti
Aprili 11, 2017.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalumu Kilimanjaro Mhe. Shally Raymond nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma wakati wa Bunge la Bajeti linaloendelea Dodoma tarehe 11 Aprili 2017. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA).
Toa Maoni Yako:
0 comments: