Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kusadia timu ya taifa ya wanawake ya Kilimanjaro Queens, ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchini. Kulia ni Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sebastian Nkomwa na Nahodha, Sophia Mwasikili.
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya wanawake ya Kilimanjaro Queens Sebastian Nkomwa akiongea mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kukabidhi vifaa va michezo kwa timu hiyo ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchini. Kushoto Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde na Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa vifaa vya michezo kwa timu ya taifa ya wanawake ya Kilimanjaro Queen kwa lengo la kuiwezesha timu hiyo kuwa na vifaa bora vitakavyowawezesha kuendelea kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi

Vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na viatu vya mpira pair 20 na socks pair 40 vitawawezesha wachezaji hao kuondoka na changamoto ya vifaa vya michezo hususani viatu bora vya kuchezea mpira ambavyo ni nyenzo muhimi katika mchezo wa soka.

Akiongea baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kwa niaba ya timu ya Kilimanjaro Queens, Mwenyekiti wa soka la wnawake Amina Karuma alisema “ Tunajisikia furaha kupokea vifaa hivi na nawapongeza sana Airtel kwa kutimiza ahadi yao yakutupatia vifaa lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kukuza soka la wanawake nchini. Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchochea kukua kwa soka la wanawake kwa kushirikisha timu za wasichana katika michuano ya Airtel Rising Stars kila mwaka na kwa kupitia michuano hii tumeweza kupata vipaji tunavyoviona leo katika timu zetu za wanawake.

“Tunawahakikishia vifaa hivi vitatusaidia saana kwani viatu vya mpira ni nyenzo muhimu sana lakini pia ni moja kati ya changamoto kubwa kwa wachezaji wetu. Tunayo mipango mingi na michuano mbalimbali iliyopo mbele yetu na tumejipanga kufanya vizuri lakini pia kujiandaa vyema kwa michuano ya AFCON inayotegemea kuanza Februari Mwakani. “Aliongeza Karuma

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema “ katika kuhakikisha tunaendeleza kukuza soka la wanawake nchini tumeona ni vyema kuwapatia wachezaji wa timu ya taifa ya Kilimanjaro Queen vifaa hivi ili kuwapa motisha ya kuendelea kufanya vizuri zaidi lakini pia kutekeleza adhima yetu ya kukuza mpira wa wanawake nchi. Tunapenda kuwapongeza sana Kili Queen kwa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ikiwemo michuano ya CECAFA ambapo timu hii iliibuka kuwa washindi na hivyo Airtel kuahidi kuwapatia vifaa ili kuendelea kuboresha kiwango chao cha mpira”

Tunajisikia furaha kutimiza ahadi hii na ni matumaini yetu vifaa hivi vitatumika vyema kwenye michuano mingi ijayo katika mwaka huu pia. Aliongeza Matinde

Kikosi cha Kilimanjaro Queens kinajengwa na wachezaji 8 walioibuliwa kutoka katika michuano yakukuza vipaji vya mpira kwa vijana ya Airtel Rising Stars yanayodhaminiwa na kuendeshwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kila Mwaka.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: