Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kushoto), akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ( kushoto), akiangalia video inayoonyesha jinsi ya kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia kamera maalum, wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
Mtaalamu wa mifumo ya Komputa , Boris Derygin akitoa maelezo kuhusu mada inayohusiana na udhibiti wa uhalifu wa mitandao wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP Gabriel Mukungu. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
Mtaalamu wa mifumo ya Komputa, Boris Derygin ,akionyesha karatasi inayoelekeza jinsi ya kuitambua gari iliyofanya uhalifu wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi , SACP Gabriel Mukungu wa Jeshi la Polisi la Tanzania, akielekezwa na Kapteni Vasily Gerasimov wa Wizara ya Ulinzi nchini Urusi, namna ya kudhibiti uhalifu katika majengo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya nchi hizo. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: