Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge wa pili kulia,akikata utepe jana wakati wa uzinduzi wa kituo cha Internet Cafe katika kikosi cha 842 KJ Mlale kilichopo wilayani Songea,kulia ni mkuu wa kikosi hicho meja Absolomon Shausi. Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Songea Mhe. Palolet Mgema,mwakilishi wa mkuu wa jeshi la Kujenga taifa Kanali John Mbungo na kushoto ni kaimu mkuu wa Brigedi ya 401 Songea, Meja Absolomon Shausi
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge akikagua gwaride rasmi la vijana 1365 waliojiunga na mafunzo ya kijeshi ya miezi mitatu katika kikosi cha 842 Kj- Mlale Jkt kwa mujibu wa sheria operesheni Magufuri 2016 kilichopo wilayani Songea
Baadhi ya vijana wa operesheni Magufuri 2016 waliojiunga na mafunzo ya kijeshi ya miezi mitatu katika kikosi cha 842 Mlale Jkt wakipita kwa mwendo wa kasi mbele ya mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge(hayupo pichani) wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo hayo jana.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge katikati akizindua Jarida la Mlale leo linalochapishwa na kikosi cha 842 KJ Mlale JKT kilichopo katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni kaimu mkuu wa kikosi hicho Meja Absolomon Shausi,wa pili kulia mkuu wa wilaya ya Songea Mhe. Palolet Mgema na mwakilishi wa mkuu wa Jkt Kanal John Mbungo.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa baraza la ulinzi na usalama la mkoa wa Ruvuma na maafisa wa mbalimbali wa JWTZ NA JKT mara baada ya kufunga rasmi mafunzo ya kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana 1365. Picha zote na Muhidin Amri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: