Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnite akizungumza aliyeambatana na Wabunge toka Sweden walipotembelea Ofisini kwake mapema leo.
Kiongozi wa ujumbe toka Sweden Bi. Matilda Irnkarns (kushoto) akikabidhi zawadi yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo
Kutoka kushoto ni Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnite akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mashaka Gambo pamoja na Kiongozi wa msafara wa wabunge toka Sweden Bi. Bi. Matilda Irnkarns kwenye picha ya pamoja baada ya Kikao
Katika picha ya pamoja ni kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Kwitega, Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnite , Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo, kiongozi wa msafara wa wabunge toka Sweden Bi. Matilda Irnkarns, ujumbe toka Sweden pamoja na viongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Baadhi wa wabunge toka Sweden wakifuatilia kikaa wakati walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema leo.
---
Nteghenjwa Hosseah –Arusha

MKOA wa Arusha umeanza kujipanga katika utaratibu wa kulinda mji kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya CCTV – Camera ili kuimarisha usalama wa mji  “Safe City”, Mfumo huu utawezeshya Mji kulindwa masaa 24 dhidi ya  uhalifu kwa raia, wawekezaji na watalii.

Kauli hiyo ilitolewa  leo mjini hapa na Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Gambo ofisini kwake mara baada
ya kutembelewa na Balozi wa Sweden nchini, Bi. Katarina Rangnite  aliyeambatana na Ujumbe wake wa Wabunge kutoka Nchini Sweden.

Akizungumza na ujumbe huo RC Gambo alisema, mkoa huo tayari umekwisha kuonyesha nia
ya kuwekeza katika mfumo huo ili kuwaongezea wananchi na mali zao  usalama zaidi.

“Nia yetu ni kuona hali ya usalama katika mkoa  wa Arusha ikiwa ya juu sana ili kuendelea kuwavutia watalii zaidi  kutoka nchi mbalimbali Duniani. Malengo yetu ni kuwa na mifumo  itakayoulinda mkoa wetu kwa Saa 24 na mwaka mzima,” alisema RC Gambo na kuongeza:

“Hatua hii itaongeza ulinzi kwa raia na mali zao,  pia kwa wawekezaji waliopo mkoani kwetu na watalii wanaokuja kutembelea  hifadhi na vivutio mbalimbali kwani Arusha ndio kitovu cha utalii hapa  nchini,” alisema.

Kwa upande wake Balozi Rangnite ambaye  kiongozi wa msafara huo uliojumuisha pia wabunge kutoka Bunge la Sweden  wanaowakilisha Kamati ya Kilimo na Mazingira, alikubaliana na nia ya  kuwekeza kwenye mfumo wa usalama wa mkoa wa Arusha.

Balozi  Rangnite alimueleza Mkuu wa Mkoa Gambo kwamba, nchi ya Sweden inayo  wataalamu waliobobea katika mifumo hiyo ya usalama wa miji hivyo  alimuomba Gambo kuwasilisha kwake maandiko ya vitu vinavyohitajika ili  kuwezesha mradi huo kutekelezwa.

“Tukipata maandiko mbalimbali  ya mradi tunaweza kuangalia ni wapi Serikali ya Sweden inaweza kuwekeza  ikiwamo kusaidia kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili,” alisema  Balozi Rangnite.

Aidha Gambo alitoa ombi kwa Balozi wa Sweeden  kushirikiana na Mkoa wa Arusha kwenye Kampeni ya Kulinda vyanzo vya Maji ili kuwezesha mradi mkubwa wa maji unaosimamiwa na mamlaka ya maji safi na maji taka (AUWSA) kutekelezwa kwa mafaniko makubwa. Itakumbukwa  kwamba imepatiwa Bil 476 ili kumaliza tatizo la maji Jiji hapa.

Katika ziara ya ujumbe huo pamoja na mambo mengine ulikuwa na lengo la  kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji katika Kilimo, Mazingira na  maeneo muhimu kutoka mkoani Arusha.

Ujumbe huo kutoka Sweden ukiongozwa na Balozi Rangnite uliridhishwa na kuvutiwa na maeneo ya
utalii yaliyopo katika mkoa huo yakiwamo pia mazingira rafiki  yanayoruhusu uwekezaji kwa jamii yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: