Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Jumatano, Aprili 15, 2026, akupewa maelezo juu ya mradi wa jengo la maabara ya TEHAMA ambayo ni ‘Smart Class’ alipokuwa Mgeni rasmi katika Mahafali ya 59 ya Shule ya Sekondari Kibaha (KSS) kama mgeni rasmi, katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Tumbi, Kibaha Mji, mkoani Pwani.
Janjaa: Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Jumatano, Aprili 15, 2026, akikagua na kupewa maelezo juu ya maabara ya TEHAMA ambayoni ‘Smart Class” na Mkuu wa Shule hiyo alipokuwa Mgeni rasmi katika n Mahafali ya 59 ya Shule ya Sekondari Kibaha (KSS) kama mgeni rasmi, katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Tumbi, Kibaha Mji, mkoani Pwani.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Jumatano, Aprili 15, 2026, akimpongeza na kumshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege (TAA) Bw. Abdul Mombokaleo kwa kujitolea computer zenye thamani ya shilingi milioni 170 kama mchango wake yeye na Alumni wengine kwa kuboresha elimu ya Sayansi katika shule hiyo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Jumatano, Aprili 15, 2026, akiwatambulisha baadhi ya Alumni walio katika kamati ya mradi wa ujenzi wa jengo la maabara ya TEHAMA ambayo ni ‘Smart Class’ katika Mahafali ya 59 ya Shule ya Sekondari Kibaha (KSS) kama mgeni rasmi, katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Tumbi, Kibaha Mji, mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege (TAA) Bw. Abdul Mombokaleo, akifuatiwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Nchini Prof. Hamisi Malebo.
Sehemu ya wahitimu wa kidato cha sita katika Mahafali ya 59 ya Shule ya Sekondari
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete, Jumatano, Aprili 15, 2026, amehudhuria Mahafali ya 59
ya Shule ya Sekondari Kibaha (KSS) kama mgeni rasmi, katika hafla
iliyofanyika shuleni hapo, Tumbi, Kibaha Mji, mkoani Pwani.
Akiwa
katika mahafali hayo, Dkt. Kikwete amezindua harambee ya kuchangia
ujenzi wa jengo la ghorofa la maabara ya TEHAMA na masomo mengine,
ambalo linatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 3.
Amesema
ujenzi huo ni muhimu katika kuendeleza ubunifu na uwezo wa wanafunzi
katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM).
Aidha,
Dkt. Kikwete amekubali kuwa mlezi wa kamati ya kukusanya michango kwa
ajili ya mradi huo mkubwa ambao kwa sasa umefikia hatua ya msingi.
Pia,
Rais Mstaafu ameishukuru jumuiya ya wanafunzi wa zamani (alumni) wa
shule hiyo, wakiuongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA) Bw. Abdul Mombokaleo, kwa kuchangia kompyuta zenye
thamani ya Shilingi Milioni 170 kwa ajili ya “Darasa Janja” (Smart
Class) lililoanzishwa shuleni hapo.
Darasa
hilo litakuwa ni kituo cha mafunzo kwa wanafunzi wa shule hiyo na shule
nyingine zitakazounganishwa kupitia mfumo wa mtandao, ambapo mwalimu
anaweza kufundisha madarasa yaliyoko nje ya Kibaha kwa wakati mmoja kwa
njia ya kidigitali.
Katika
ziara yake, Dkt. Kikwete alipata fursa ya kutembelea na kukagua Darasa
Janja hilo, akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Shule kuhusu namna
teknolojia hiyo inavyotumika kuboresha mbinu za ufundishaji na
ujifunzaji shuleni hapo.
Shule
ya Sekondari Kibaha, inayomilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha na
kusimamiwa na Kurugenzi ya Hud uma za Elimu, ilianzishwa mwaka 1965
kupitia ushirikiano kati ya Serikali ya Tanganyika ya wakati huo na nchi
za Nordic – Denmark, Finland, Norway, na Sweden. Wakati inaanzishwa,
shule ilikuwa na wanafunzi 110 wa Kidato cha Kwanza na 60 wa Kidato cha
Tano.
Kwa
sasa, shule hiyo ya bweni kwa wavulana ina uwezo wa kuchukua zaidi ya
wanafunzi 800 na imeendelea kuwa miongoni mwa taasisi kongwe na zenye
heshima kubwa katika sekta ya elimu nchini.
Dkt.
Kikwete ni miongoni mwa alumni mashuhuri wa Shule ya Sekondari Kibaha,
alikosoma zaidi ya miaka 60 iliyopita. Wengine waliopitia shule hiyo ni
pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Bw.
Peter Ulanga, Balozi Lazaro Nyalandu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa
ya UNESCO Nchini Prof. Hamisi Malebo, Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya
Ndege Bw. Abdul Mombokaleo, na Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA Mhe.
Freeman Mbowe, miongoni mwa wengine wengi.
Aidha,
kwa kutambua mchango mkubwa wa alumni wake, Shule ya Sekondari Kibaha
inaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wa elimu ili kuhakikisha
inaendelea kuwa kinara katika utoaji wa elimu ya ubora nchini.
Kibaha, Katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Tumbi, Kibaha Mji, mkoani Pwani. (Picha na Habari na Issa Michuzi)
mm







Toa Maoni Yako:
0 comments: