Mhe. Grace Ngowi Jungulu akionesha zawadi ya kitabu cha Mungu Biblia aliyozawadiwa na watumishi wake wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru wanachama na wananchi waliojitokeza kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Serikal Oktoba 29 mwaka huu.

Na Mwandishi Wetu, KIBAHA 

Mhe. Grace Ngowi Jungulu amesema sasa ni muda wa kazi na milango ya nyumba yake ipo wazi, pale wanapoona kuna tatizo wasisite kumpigia simu au kufika nyumbani kwake.

Jungulu amesema, yeye amechaguliwa na wananchi wa Kata ya Picha ya Ndege, hana budi kuwatumikia na hilo atalifanyika kwa uwezo wake wote.

Hayo ameyasema Diwani wa Kata ya Picha ya Ndege Mhe. Grace Ngowi Jungulu wakati wa kuuwashukuru wanachama wote wa CCM na wananchi wa Kata ya Picha ya Ndege baada ya kumchagua na kushindwa kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali uliofanyika Oktoba 29, mwaka 2025.

Akizungumza na wananchi wake wakati wa hafla fupi baada ya kuapishwa, Mhe Jungulu amesema anashukuru kwa ushindi aliopata anaamini yale aliyoyaanza kuyafanya akiwa Mwenyekiti wa CCM Kata ataenda kuendelea kuyamalizia kwa sababu tayari ameshapata nafasi ya kuwasilisha changamoto zote kwenye Serikali Kuu.

Mhe. Jungulu amesema, Kata ya Picha ya Ndege imeweza kumuamini na kumpa nafasi hiyo ya kuwatumikia na anawaahidi kuwa atatimiza yale yote aliyowaahidi wakati wa kampeni.

Aidha, katika hafla hiyo fupi, Mhe Jungulu amewaomba Vijana kutokengeuka na kufuata mkumbo ambao utakuja kuchafua amani iliyopo Kata ya Picha ya Ndege.

"Leo hii mimi nikiwa Diwani wa Kata ya Picha ya Ndege, nawaambia kuwa vijana msije mkajaribu kukengeuka na kufuata mkumbo wa kutuondolea amani iliyopo ndani ya Kata yetu, sitaruhusu hilo litokee,"amesema Jungulu 

Amewataka wananchi kulinda amani ya Picha ya Ndege na kusema yeye akiwa kama Diwani yupo tayari kushirikiana nao kwenye nyakati zote , namba zake zipo hewani hata milango ya nyumba yake ipo wazi pale wanapokuwa wanahitaji kuzungumza nae.

Pamoja na yote, Mhe Jungulu amewashukuru wafanyakazi wake ambao waliweza kumzawadia Kitabu cha Biblia pamoja na picha ya Bikira Maria na wamemtaka kutumia muda wake mwingi kumuomba Mungu amuongoze kwenye shughuli zake za kila siku.

Tarehe 04/12/2025 ilikua ni siku ya uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mjini ambapo madiwani 19 na tayari kuanza kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kibaha Mjini.
Mhe Grace Ngowi Jungulu akisaini baada ya kumaliza kuapa na kuwa Diwani kamili wa Kata ya Picha ya Ndege. 
Wananachi na wafanyakazi wakiwa na furaha. 



Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: