Morogoro, Jumamosi, 6 Desemba 2025 — Msanii nguli wa muziki wa Bongo Flava, Afande Sele, anatarajiwa kuandika historia mpya leo baada ya kuamua kuingia rasmi katika maisha ya ndoa na mchumba wake, mwandishi wa habari Imani Makongoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Kamati ya Harusi, ndoa hiyo imepangwa kufungwa katika eneo la Nguzo Camp jijini Morogoro, kabla ya wageni kuelekea kwenye tafrija itakayofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Morena.

Sherehe hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wadau mbalimbali wa muziki na vyombo vya habari.

Afande Sele, ambaye anatambulikana na wengi kama “Mfalme wa Rhymes Tanzania”, amekuwa mmoja wa wasanii wenye mchango mkubwa katika muziki wa hip hop nchini, huku mchumba wake Imani Makongoro akiwa miongoni mwa waandishi chipukizi wenye taswira pana katika uandishi wa habari.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: