Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya soka, Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa droo ya mzunguko wa awali ya CAF Champions League na Confederation Cup, itakayofanyika Agosti 9, 2025, jijini Dar es Salaam. Tukio hili linaifanya Tanzania kuendelea kung’ara katika ramani ya soka Afrika.
Droo hiyo inakuja wakati ambapo michuano mikubwa ya CHAN 2025 (Kombe la Mataifa kwa Wachezaji wa Ndani) inaendelea kwa kishindo katika ukanda wa Afrika Mashariki, ikihusisha nchi tatu mwenyeji: Kenya, Tanzania na Uganda. Hii ni mara ya kwanza kwa ukanda huu kuwa mwenyeji wa pamoja wa michuano hiyo ya CAF, jambo linaloashiria kuimarika kwa miundombinu na umaarufu wa soka katika eneo hilo.
10 BORA VILABU VYA CAF 2025:
1.Al Ahly SC (Misri) – Pointi 78
2. Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) – Pointi 62
3. Espérance de Tunis (Tunisia) – Pointi 57
4. RS Berkane (Morocco) – Pointi 52
5. Simba SC (Tanzania) – Pointi 48
6. Pyramids FC (Misri) – Pointi 46
7. Zamalek SC (Misri) – Pointi 42
8. Wydad AC (Morocco) – Pointi 39
9. USM Alger (Algeria) – Pointi 37
10. CR Belouizdad (Algeria) – Pointi 36
TANZANIA YAING’ARA:
● Simba SC – Nafasi ya 5, Pointi 48
● Young Africans (Yanga SC) – Nafasi ya 12, Pointi 34
Vilabu hivi vinaendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa, huku Simba ikiingia kwenye tano bora kwa mara ya kwanza katika historia ya CAF Club Rankings.
UMUHIMU WA DROO NA CHAN KUWA TANZANIA:
Uamuzi wa CAF kuifanya Tanzania kuwa mwenyeji wa droo ya mashindano, sambamba na michuano ya CHAN 2025, ni ushahidi tosha wa nafasi ya juu inayopata Tanzania katika maendeleo ya soka barani. Tukio hilo linatarajiwa kuhamasisha uwekezaji zaidi kwenye michezo, kuvutia mashabiki, na kukuza utalii wa michezo.


.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments: