Julai 9, Dar es Salaam. Katika kesi ya mwandishi wa habari Eric Kabendera kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, ambapo amedai fidia ya dola milioni 10 dhidi ya Vodacom, kampuni hiyo imekanusha vikali madai hayo yaliyotolewa na Kabendera.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mtaalamu Mwandamizi wa Sheria kutoka Vodacom, Joseph Tungaraza alisema, "Tunakanusha vikali madai ya mlalamikaji. Tunatoa huduma zetu kwa wateja wetu wote kwa kuchukua hatua madhubuti za faragha ya data. Kulinda usiri na usalama wa data zote ni jambo muhimu, na tunaendelea kutekeleza taratibu zote za kisheria za kulinda taarifa nyeti za wateja ila kuhakikisha uaminifu na faragha ya wadau wetu kwa ujumla unabakia kuwa kipaumbele chetu..
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: