Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Dar es Salaam 
Serikali imekamilisha majadiliano kati yake na Kampuni ya Viettel Global Joint Stock ya Vietnam kuhusu utekelezaji wa mkataba wa ufikishaji mawasiliano ikiwepo ujenzi wa miundombinu ya mkongo ulioingiwa tangu mwaka 2014.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa vikao hivyo vya majadiliano tarehe 19 Julai, 2024, Mwenyekiti wa Timu ya Majadiliano ya Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Adolf Ndunguru amesema majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kuhusu utekelezaji wa mkataba huo yamekamilika. 
SERIKALI, VIBw. Ndunguru amesema kuwa serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari itaendelea kushirikiana na kampuni hiyo na kuhakikisha uwepo wa mazingira mazuri na wezeshi katika Sekta ya Mawasiliano.

“Leo tumehitimisha majadiliano na kampuni ya Viettel kuhusu mgogoro uliokuwepo kwa muda mrefu kwenye sekta ya mawasiliano, na majadiliano haya yamekamilika kwa kila upande kuridhika na hatua iliyofikiwa,” amesema Bw. Ndunguru.
Nae kiongozi wa Timu ya Majadiliano wa Kampuni ya Viettel Global Joint Stock Investment Bw. Phung Van Cuong ameishukuru Serikali ya Tanzania, Timu ya Serikali ya Majadiliano na Timu ya Wataalam ya Serikali kwa kukamilisha majadiliano hayo yaliyozingatia maslahi ya pande zote mbili.

“Kwa niaba ya Kampuni ya Viettel Global tunasema asante sana kwa Serikali ya Tanzania kwa kusaidia uwekezaji wetu, sisi tunaahidi kuendelea kuwekeza zaidi katika sekta ya mawasiliano, tunashukuru sana”, amesema Bw. Phung Van Cuong.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: