WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema Serikali inaendelea na maandalizi ya utekelezaji wa Gridi ya Taifa ya Maji inayolenga kutumia vyanzo vya uhakika vya maji ikiwemo maziwa na mito.

Ameyasema hayo leo April 23, 2024,jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Buhigwe Kavejuru Felix aliyeuliza Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Mradi wa Grid ya Maji ya Taifa kwa kutoa maji Ziwa Victoria na Tanganyika.

Aweso amesema kwa sasa hatua iliyofikiwa ni ya kuajiri Mtaalam Mshauri atakayefanya upembuzi yakinifu wa mpango huo anatarajiwa kuajiriwa katika mwaka wa fedha 2024/25.

"Aidha,Serikali imeanza kutumia vyanzo vikubwa vya maji vya uhakika ikiwemo maziwa, mito mikubwa na mabwawa kwa ajili ya kusambaza huduma ya maji kwenye maeneo ambayo hayana vyanzo vya uhakika vya maji. Mfano ni mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ambao umenufaisha Miji ya Kahama, Shinyanga, Tinde, Nzega, Tabora, Igunga na Shelui."amesema Aweso
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: