●Ikiwa ni mojawapo ya eneo lililopendekezwa zaidi kuwa thabiti na muhimu kwa shughuli za uwekezaji barani, Tanzania inajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa tano wa mwaka wa kimataifa wa Tanzania Energy Cooperation Summit (TECS) utaofanyika kuanzia Januari 31 mpaka Februari mosi, 2024 jijini Arusha, nyumbani kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC). 

---

Dar es Salaam - Desemba 22, 2023. Wawekezaji kutoka sekta mbalimbali, fedha na serikali zitakutana kuonyesha uwezo ilionao Tanzania.

Uwezo ambao unaonyeshwa na nchi ambayo kwa sasa imeorodheshwa kuwa ya tatu kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uwekezaji siku za mbeleni, ambapo inatarajiwa kuona ukuaji wa Pato la Taifa kwa 6% ifikapo 2025, huku ikishuhudia mamia ya mamilioni, kama sio mabilioni, ya uwekezaji wa dola, unaolenga kuelekezwa kwenye miundombinu, umeme wa maji, gesi asilia (LNG) na miradi ya nishati ya jua katika miaka ya hivi karibuni. 

Ikiwa imeorodheshwa na KPMG ikiwa nyuma ya nchi za Afrika ya Kusini na Nigeria, Tanzania imejithibitishia hadhi yake yanapokuja masuala ya biashara na uwekezaji. 

Taifa lilitajwa kwa eneo lake la kimkakati mashariki mwa bara la Afrika, wingi wa maliasili, na ongezeko la uwekezaji hivi karibuni, haswa katika sekta ya nishati. Kiwanda cha kwanza cha umeme wa jua cha 50MW kwenye gridi ya taifa, uwekezaji wa dola za Marekani milioni 300 katika nishati ya maji, mradi wa gesi asilia wa dola bilioni 42 ulioanzishwa na Shell, Equinor na Exxon Mobil, na takribani dola za Marekani bilioni 7 zilizoingizwa kwenye miundombinu, inathibitisha mvuto wake barani Afrika na kimataifa.

Ukiwa umeratibiwa na EnergyNet, mkutano wa kimataifa wa TECS24 hautoainisha mafanikio haya ya kujivunia pekee bali itaangazia fursa zijazo za biashara na miradi ya uzalishaji inayotarajiwa kubadilisha nchi na ukanda huu zaidi. Changamoto zinazohusiana na fedha na dhamana pia zitajadiliwa, ili kuchochea ari zaidi ya majadiliano na kuhakikisha sekta ya umeme nchini inaendelea kuimarika zaidi.

Pamoja na wawekezaji wakubwa, wadau watakaohudhuria ni pamoja na mawaziri wa kitaifa kutoka Tanzania, Malawi, na Ethiopia, pamoja na viongozi wa makampuni ya utoaji huduma ya kitaifa, ikiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO wa Tanzania, Gissima Nyamo-Hanga. Wasemaji kutoka Electricidade de Moçambique (EDM) na ZESCO ya Zambia pia watakuwepo. Wao, pamoja na wawakilishi kutoka sekta za umma na binafsi, wakurugenzi kutoka taasisi za kifedha - ikiwa ni pamoja na AfDB, BII, World Bank Group na ATIDI - na mashirika ya kikanda, wote watakuwepo Arusha, kwa ajili ya mkutano wa biashara wa hadhi ya juu wa aina yake.

Kwa kuzingatia nafasi ya Tanzania kama mhimili wa nishati kikanda, mada zitakazojadiliwa ni pamoja na mtazamo wa kiuchumi wa Tanzania na uwezo wa maendeleo ya nishati, pamoja na kupanga njia bora ya kujenga soko la umeme la kikanda. Ushirikiano wa sekta za umma na binafsi katika miradi ya usafirishaji pia utakuwa kwenye ajenda, pamoja na wakurugenzi kutoka taasisi za kifedha, utawala na kanuni, na nafasi muhimu ya nishati mbadala. Washiriki watapewa fursa ya kutoa mawazo kuhusu kutengeneza uunganisho bora wa kikanda, mifumo imara zaidi kwa biashara na uwekezaji, na hatimaye kuunda ramani ya ufikiaji wa nishati kikanda kwa siku za usoni. 

"Tanzania imejitengenezea nafasi muhimu kwa biashara barani. Kwa kuwa na uhusiano baina ya kusini na mashariki na pia ulimwenguni kote, nchi hii siku zote imekuwa na uwezo wa kuwa mwanzilishi wa ukuaji wa viwanda - na sasa tunashuhudia jinsi adhma hii itakavyotimizwa. Hivyo nina shauku kubwa kuonyesha ukuaji wa Tanzania kuhakikisha fursa na kasi hii inaendelea," alisema Simon Gosling, Mkurugenzi Mtendaji, EnergyNet. 

Aliongeza, "Pia tunafurahi kuandaa mkutano huu Arusha, ukitoa muda na nafasi kwa kila mtu kujadili kwa kina masuala muhimu zaidi kuhus sekta mbalimbali."

"Tanzania akiwa mmojawapo wa nchi waanzilishi wa Jumuiya yetu, tuna nia ya dhati kuiunga mkono zaidi kusaidia malengo yake kwenye sekta ya nishati. Tukiendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mkutano wa mwaka jana uliofanyika Dar es Salaam, tunatumaini kuwa TECS24 itatoa ufafanuzi zaidi kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika sekta ya nishati na jinsi wakurugenzi kutoka taasisi za kifedha - hasusani watoaji wa bima na dhamana wa kikanda kama vile ATIDI - wanaweza kusaidia juhudi hizo na mabadiliko makubwa ya nishati kwa ujumla," alisema Obbie Banda, Mchambuzi na Kaimu Mratibu wa Regional Liquidity Support Facility (RLSF) katika taasisi ya African Trade and Investment Development Insurance (ATIDI).

Aleem Tharani, Mkuu mwenza wa Infrastructure Sector Group (Afrika), Bowmans na Mkuu wa Miradi, Nishati na Miundombinu (Afrika), alihitimisha: "Mkutano wa 5 wa kimataifa wa Tanzania Energy Cooperation Summit unaweka alama muhimu kwa sekta ya nishati barani Afrika. Kwa kuwaunganisha wawekezaji, taasisi za serikali na wataalamu wa sekta, tunachochea majadiliano muhimu kwa ajili ya kukuza ramani ya nishati ya Tanzania, kutoa kipaumbele kwa gesi na nishati mbadala, na kuboresha usafirishaji wa kikanda. Bowmans inajivunia kudhamini mkutano huu, ikiona umuhimu wake katika kuunda mustakabali wa nishati wa Afrika na kuzidisha ushirikiano wa umma na binafsi."  

Angalia ajenda na orodha ya wasemaji hapa https://www.tanzania-ecs.com/

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: