Meneja Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa Self Microfinance Fund uliopo chini ya Wizara ya fedha, Bi. Linda Mshana akiongea na waandishi wa habari katika Maonyesho ya tatu ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa yanafanyika mkoani Arusha, kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abed Jijini, Arusha.
Afisa mikopo kutoka Self, Bw. Mbwana Msangule akiendelea kuwapa elimu wateja walioudhuria katika banda lao lililopo katika Maonyesho.

Na Mwandishi Wetu, ARUSHA.

Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupata elimu kuhusiana na masuala ya fedha ili iwasaidie kutimiza malengo yao na kukuza uchumi kwa ujumla.

Ili kuepuka matatizo ya kuuziwa mali, kutokana na kushidwa kurejesha mikopo wanayochukuwa katika taasisi mbalimbali.

Hayo yamebainishwa na Meneja Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa Self Microfinance Fund uliopo chini ya Wizara ya fedha, Bi. Linda Mshana wakati akiongea na waandishi wa habari katika Maonyesho ya tatu ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa yanafanyika mkoani Arusha, kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abed Jijini, Arusha.

Bi. Linda Mshana amesema kuwa chanzo ni kutokuwa na uelewa wa kutosha pamoja na elimu ya duni ndicho kinachopelekea baadhi ya Watanzania kushindwa kurejesha mikopo mbalimbali kwani wengi wao wamekuwa wakifanya maamuzi pasipo kuwa na uelewa wa kutosha katika eneo hilo.

Amebainisha kuwa kulingana na mahitaji ya mikopo na kuongezeka kwa utitiri wa taasisi za mikopo, vijana wa Kitanzania wanashauriwa kuungana na kukopa kwenye taasisi za fedha za kuaminika na zenye usimamizi wa serikali ili kuepuka fedhea katika mikopo hiyo huku akiwasihi kupata elimu ya kutosha kabla ya kuichukuwa mikopo hiyo.

Aidha ametaja aina za mikopo ambayo inatolewa na mfuko wa SELF Microfinance ni mkopo wa Kilimo, Biashara, Makazi, mkopo wa pamoja, mkopo wa Imarika, Mkopo wa Mahitaji na mikopo wa Mkulima ambapo pia alifafanua kuwa nia yao ni kuendela kuwapatia watanzania elimu na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini.

Amesema kuwa kila Mtanzania ana fursa kubwa ya kupata mkopo na kujikuza kiuchumi, kwa wajasiriamali wote wachini, wa kati, wakubwa, wafanyakazi,na watuwanaotaka kuboresha makazi.

“Wale waliopo kwenye vikundi wanaotaka mikopo ya kujiinua kiuchumi, wasiache fursa zikawapita, tunawafanyakazi waliokidhi na wana weledi wakuhudumia wajasirimali wote wanaotaka kujinua kichumi wafike tu katika matawi yetu yalipo katika mikoa mbalimbali ikiwemo hapa Arusha katika jengo la hazina ,Mwanza ,Dodoma,Dar es Salaam, Mbeya, Kahama, Geita, Morogoro, Tanga, Mtwara, Iringa pamoja na Zanzibar kupata elimu ya kutosha kuhusiana na mikopo namna ya kurejesha pamoja na riba" amebainisha Linda.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: