Kikosi kazi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Kilimo, Ofisi ya Rais Tamisemi kimefanya ziara na kufanya mazungumzo na Kaimu Afisa Tawala Msaidizi sehemu ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Bwana Lusungu Esau Mdede Mkoani Njombe.
Lengo la ziara hiyo kufanya tathimini ya namna bora mazao ya kilimo yanavyoweza kufungashwa kwa kufuata vipimo sahihi.

Aidha, Bwana Mdede amesema ujio wa kikosi kazi hiki ni tumaini na suluhisho kwa wakulima kwani wengi wamekuwa na hamasa ya kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo kwani itasaidia katika upatikanaji wa faida zaidi na kuepukana na matumizi ya madebe na visado katika mazao ya kilimo hususani nyanya, vitunguu, karoti, tangawizi na viazi mviringo.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya maendeleo ya biashara Dkt. Hanifa Mohammed Yusuph amesisitiza kuwepo na matumizi sahihi ya vipimo katika mazao kilimo ni muhimu ili kuwezesha upatikanaji wa mapato Serikalini na kukuza ustawi wa biashara nchini.

Wakati huohuo wakulima na wafanya biashara mkoani Njombe wamepewa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya vipimo ili kuepuka hasara na pia adhabu mara watakapobainika kukikuka sheria ya vipimo nchini.

Kikosi kazi hiki kimeanza tathimini hii tarehe 13 Novemba, kikipitia katika masoko ya jiji la Dar es salaam, Arusha, Manispaa ya Iringa na mkoa wa Njombe kwa lengo la kutathmini ufungashaji wa mazao ya kilimo yasiyofuata vipimo sahihi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: