Matawi mbalimbali ya benki ya CRDB Kanda ya Ziwa yamejumuika pamoja kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, ambayo huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba ambapo watoa huduma hujumuika pamoja na wateja ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wao.
Ufunguzi wa maadhimisho hayo umefanyika Jumatatu Oktoba 02, 2023 katika tawi la benki ya CRDB tawi la Mwanza kwa niaba ya matawi mengine ya benki hiyo Kanda ya Ziwa na kuhudhuriwa na wafanyakazi pamoja na wateja wa CRDB.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta amesema benki hiyo imejipanga kuwahudumia wateja wake kupitia huduma mbalimbali ambazo ni pamoja na huduma za kidijitali ambazo zimeifanya kuwa benki kinara.
"Mwaka huu benki yetu imetambulika na kutunukiwa na taasisi ya utafiti ya 'European Society' kama benki bora inayotoa huduma nzuri kwa wateja wake hivyo tunaungana na wateja wateja kujivunia hilo. Benki ya CRDB inatoa huduma kidijitali, mlio wengi mnatumia Sim Banking, Internet Banking, Sim Account na Mawakala ambapo huduma zote hizo zinatusaidia kutoa huduma nzuri na kuwa benki kinara" amesema Sitta.
Pia Sitta ameongeza kuwa benki ya CRDB inatoa huduma mbalimbali utunzaji akiba, utoaji mikopo, bima aina zote pamoja na amana za uwekezaji (kijani bond/ hati fungani) zinazotoa fursa kwa wateja kufikia matarajio yao kiuchumi.
Nae mgeni rasmi, Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi ameipongeza benki ya CRDB kwa kutoa huduma bora zinazoendana na matarajio ya wateja wao.
"Utoaji huduma bora ni msingi wa kuboresha biashara na maisha ya watu ndiyo maana Serikali inasisitiza utoaji huduma bora kwa wananchi ambapo taasisi za kifedha ikiwemo benki ya CRDB zina wajibu wa kuendelea kutoa huduma bora kwa uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla" amesema Salala.
Pia Salala ametoa rai kwa benki ya CRDB kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kutambua umuhimu wa kujiunga na huduma za bima kwani bado mwitiko uko chini. Aidha maetoa rai kwa wateja kutumia wiki ya huduma kwa wateja kutoa maoni yatakayosaidia benki ya CRDB kuboresha zaidi huduma zake.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta akizungumza kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniano uliofanyika Jumatatu Oktoba 02, 2023 katika tawi la CRDB Mwanza kwa niaba ya matawi mengine ya benki hiyo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Maadhimisho hayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa wateja.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Thomas Salala akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (hayuko pichani) kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yaliyofanyika Jumatatu Oktoba 02, 2023 katika tawi la CRDB Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana- Thomas Salala (katikati), Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa- Lusingi Sitta (kulia) na mwakilishi wa wateja wa benki ya CRDB (kushoto) wakikata keki kwenye maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani yaliyofanyika katika tawi la CRDB Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala (kulia) akimlisha keki mmoja wa waeja wa benki ya CRDB wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Waeja Duniani yaliyofanyika katika benki ya CRDB tawi la Mwanza.
Mteja wa benki ya CRDB jijini Mwanza (kulia) akimlisha keki Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani yaliyofanyika katika benki ya CRDB tawi la Mwanza
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta (kulia) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi, Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala (kushoto) aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (hayuko pichani).
Mgeni rasmi, Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta (kulia) wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani yaliyofanyika katika benki ya CRDB tawi la Mwanza.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala (wa pili kushoto waliokaa).

Wateja na wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala (wa pili kushoto waliokaa) wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani yaliyofanyika katika benki ya CRDB tawi la Mwanza.

Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiwa kwenye maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani yaliyofanyika katika benki ya CRDB tawi la Mwanza.

Wateja wa benki ya CRDB wakijumuika na wafanyakazi wa benki hiyo kupata kifungua kinywa pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments: