Baadhi ya wachezaji wakipambana katika mashindao ya E4M Social Centre ambayo yamechezwa katika kata ya Kitwiru mtaa wa Kibwabwa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Naibu meya wa manispaa ya Iringa Kenyetta Likotiko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika fainali ya mashindano ya E4M social centre siku ya kesho tarehe 27/03/2022 katika kiwanja cha kimata kilichopo mtaa wa Kibwabwa kata ya kitwiru Manispaa ya Iringa kwa mchezo kati ya timu ya Kibwabwa Fc na timu ya Dabalidali Fc ambazo zote zinatoka katika kata ya Kitwiru.

Akizungumza na blog hiii mdhamini wa mashindano hayo, Ibrahim Alex Manager E4M Sports Club alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kutafuta wachezaji ambao wataunda timu moja kwa ajili ya kuanza kucheza ligi ya TFF ngazi ya wilaya hadi kupanda ligi kuu hapo baadae.

Alex alisema kuwa wamekuwa wakijihusisha na maswala ya michezo hivyo hivi sasa wamejipanga kuhakikisha wanaibua vipaji vipya ambavyo vitaisaidia timu ambayo wanatarajia kuinda mara baada ya kumaliza mashindano hayo.

Alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa na msisimuko mkubwa kwa wananchi na wadau wa michezo katika kata ya Kitwiru kwa kuwa ilishilikisha timu zote kutoka kata hiyo kwa lengo kwa kuangalia namna gani kata hiyo imebalikiwa kuwa na mipaji vya wachezaji wa mpira wa miguu.

Alex alisema kuwa jumla ya timu nane ndizo ambazo zilishirki mashindano hayo ambazo ni Kibwabwa,Dabalidabali,Mseke,Amani Center,Mnazi,Jamaica,Kitwiru na Juventus ambazo zote hizo ziligawanywa katika makundi mawili ya mashindano.

Aliongeza kwa kusema kuwa mshindi kwanza wa mashindano hayo anajinyakulia seti moja ya Jezi pamoja na mpira moja,mshindi wa pili atajinyakulia seti moja ya Jezi,mfungaji bora,kocha bora,goli kipa bora hao wote watajinyakulia kiasi cha shilingi elfu hamsini kila mmoja(50000) wakati mchezaji bora atapata kiasi cha shilingi elfu thelethini (30000).

Alex aliongeza kuwa timu yenye nidhamu itapata kreti la soda wakati mashindano yalipokuwa yanaendelea kwenye kila mchezo mchezaji bora alikuwa anapewa kiasi cha shilingi elfu tano(5000) hiyo yote ilikuwa kwa lengo la kuongeza morali ya wachezaji.

Alimalizia kwa kusema kuwa anawakaribisha wadau,wapenzi na wananachi wote katika fainali hiyo na baada ya fainali zawadi na sherehe zote zitafanyika katika ukumbi E4M Social Centre njia panda ya tosa maganga. Usafiri utakuwepo wa kuwachukua wachezaji wa timu zote 8 zilizoshiriki mashindano. Kikosi bora cha wachezaji 25 kitatajwa
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: