Mhe Abubakar Kunenge ameeleza kuwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuhakisha kuwa anaboresha maisha ya Watanzania na kuondoa kero zao kwa kuleta Ustawi kwenye shughuli za kijamii na Kiuchumi. Ameyasema hayo leo Januari 16, 2022 wakati akikagua Daraja la Mbuchi lililopo Wilayani Kibiti.

"Tunajivunia Daraja hili la Mbuchi linalojengwa kwa Gharama ya Shilingi Bilioni 6.245 litakuwa na urefu wa mita 61, pamoja na Matengenezo ya Barabara hii ya Muhoro -Mbuchi- Mbwera ya urefu wa kilometa 23 kwa sasa Ujenzi umefikia asilimia 80".

"Mhe Rais ameamua kuifungua Pwani kufika kusiko fikika" ameongeza kunenge.

Kunenge ametaja kuwa uwepo wa Daraja hilo kutachochea shughuli za kiuchumi ikiwemo utalii,Uvuvi na kilimo Biashara.

ametoa rai kwa mkandarasi kufanya kazi usiku na Mchana na kukamilisha Ujenzi kwa wakati ifikapo Februari 23, 2022

Kunenge amewataka wananchi kutojihusisha na Wizi wa vyuma vya Daraja hilo.












Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: