Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika leo tarehe 18 Januari 2022 katika ngazi ya Makatibu Wakuu jijini Kampala, Uganda.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Uganda Bw. Bagiire Vincent Waiswa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika leo tarehe 18 Januari 2022 katika ngazi ya Makatibu Wakuu jijini Kampala, Uganda.
Balozi Fatma (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz wakifuatilia majadiliano wakati wa Mkutano huo.
Kutoka Kulia ni Dkt. Hashil Abdalla Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara pamoja na Bw, Kheri Mahimbali Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati wakifuatilia majadiliano wakati wa mkutano huo.
Kutoka Kulia ni Dr. Ally Possi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) na Bw. Mohammed Addulla, Naibu Katibu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakifuatilia majadiliano kwenye Mkutano huo.
Bw. Kagiire Waiswa pamoja na Mhandisi Irene Okello Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wa Uganda wakifuatilia Mkutano.


Makatibu Wakuu na ujumbe wa Uganda wakifuatilia Mkutano.
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Uganda ikifuatilia Mkutano.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: