Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan
Waziri wa UTamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Innocent Bashungwa
Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi
Bahati Bendi ni miongoni mwa wasanii wataokuwepo.
Na John Mapepele
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa (Mb) leo Desemba 10, 2021 anazindua Mashindano ya Taifa CUP 2021 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mhe. Bashungwa amesema Serikali imeamua kufufua mashindano hayo ili kupata vipaji vya wachezaji ambavyo vitaendelezwa ili Tanzania iweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya kimataifa.
“Lengo la mashindano hayo pia ni kuwashirikisha wanamichezo kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.Tunatarajia yatasaidia kuleta umoja na mshikamano, kutoa ajira na kuimarisha afya za wachezaji wetu.
Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kurejesha mashindano hayo ambayo yalikuwa yamesimama kwa miaka kadhaa.
Aidha, amesema mashindano ya mwaka huu yameboreshwa tofauti na yale ya awali ambapo amesema maboresho hayo ni pamoja na kuingiza michezo mitatu; soka kwa wanaume na wanawake, netiboli na riadha kwa wanaume na wanawake ambapo awali ulikuwa mchezo mmoja tu wa soka.
Pia amesema mashindano haya yameshirikisha pande zote mbili za Tanzania ili kuwa na sura ya kitaifa
Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amesema uzinduzi huo utapambwa burudani kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya, michezo ya jadi na Bendi ya Muziki.
Amewataja wasanii wataotumbuiza kwenye uzinduzi huo kuwa ni pamoja na Dulla Makabila, Isha Mashauzi, Fid Q, Madee, Lucy Charles, Bahati Bendi na kikundi cha hamasa cha michezo ya jadi.
Aidha, Dkt. Abbasi amesema kuwa mechi ya mpira wa Miguu ya wanaume kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa mashindano hayo itakuwa baina ya timu ya Kaskazini Unguja na Timu ya Mkoa wa Mtwara.
Mhe. Bashungwa, ametoa rai kwa vyama vya michezo na mashirikisho kuja kwenye mashindano hayo ili kuona vipaji vya wachezaji ambao wanaweza kuwachukua kwenye vilabu vyao.
Pia amefafanua kwamba tayari Wizara yake imeandaa mkakati wa michezo ambao umeainisha michezo ya kipaumbele. Michezo ya kipaumbele inajumuisha Soka, Riadha, Ngumi, Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu na Mpira wa Pete (Netiboli).
Toa Maoni Yako:
0 comments: