Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ,Jenerali Mstaafu ,George Waitara akikabidhi tuzo iliyotolewa kwa Hidahi ya Taifa ya Serengeti kwa Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Kigwangalla wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya TGT jijini Arusha.
Na Dixon Busagaga wa Globuya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu wa Jeshi ,George Waitara leo amekabidhi kwa Waziri wa Utalii na Maliasili Dkt Khamis Kigwangalah tuzo iliyoshinda Hifadhi ya Taifa ya Serengeti baada ya kutangazwa hifadhi bora barani Afrika.
Tuzo hiyo iliyotolewa na taasisi ya World Travel Award (WTA) June Moshi nchini Mauritius baada ya Hifadhi ya Serengeti kuwa na sifa za kipekee miongoni mwao ikiwa ni idadi kubwa ya wanyama wahamao,wanayama walao nyama na uwepo wa ukanda mrefu wwenye wanyama wengi imepangwa kukabidhiwa kwa raisi Dkt John Magufuli.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo hiyo kwa Waziri Kigwangala,hafla iliyofanyika katika viwanja vya TGT yanapofanyika maonesho ya Utalii ya Karibu/Kili fair ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugnzi TANAPA ,George Waitara amesema ushindi wa Hifadhi ya Serengeti kuwa Hifadhi Bora ni ushindi wa Watanzania wote.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf Mkenda amesema tuzo hiyo imepatikana baada ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushindanishwa na Hifadhi nyingine kubwa tano barani Afrika kwa watalii kupiga kura.
Toa Maoni Yako:
0 comments: