Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) akizungumza kwa msisitizo na uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Afya na Sayansi Shiriki (UDSM -MCHAS) katika ziara yake ya kutembelea na kukagua eneo kitakapo jengwa Chuo katika eneo la Tanganyika Pekers nje kidogo ya Jiji la Mbeya .
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjALrxLpfBguZeho3pqtmifJsXUWedqi0XdPEK_7n4_cRdN5OG5ACbc6Hrq222ggj3gpzpJOUzlXDJ7DibsrIFi6PXWI-6sjo7twRS9hYYrtL0ElL1FQvRIroySnvPx3mVkIziWB3vt-ZE/s640/1.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgAnvpBu0ij4Br-cuNpv1NB4xUpczFr2LXuije33PftixCRnqXTc93WXivhLWuz1PKJO339HvlhBGsa1GkcH5ZvLzQBxdzurJAyQX3Dg5Li1MA6kB4Q-muTtKj5Jd8I8RUa5F0KeCJ3GoqB/s640/2.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNHJNzOivyqZqXgaOk9L4Zjs2JfkNibNOKwnFDxsHobG9NDh6-oSV_SvdOKuNe75gznwrLpjzqG1gKwPq8VIt09BUySMm3leW0hR8iP6sXU14tOk2cnQzJdLtDar3BzF4qeI9qRxzHAOh7/s640/3.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjy92wi8X1MjVzdENgFafVOZlwmE-20O5K0QAwQxxyIPpTHjwbtHhi3fqWA3z_3ihKGifyyx1JUIuCuriIG7sQP7AbiZ1l75UarD8dppnx1oVCPMwTBBlzgb2S3iktnvcoMqEadLAg58m1Q/s640/4.jpg)
Na Emmanuel Madafa.
MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais Mstaafu awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka watendaji wa Chuo hicho kusimamia nidhamu na ubora wa elimu ili kiwe chuo cha mfano Barani Afrika.
Rais, Kikwete aliyasema hayo jana wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama na serikali, baada ya kutembelea na kukagua eneo la ardhi lililotengwa na serikali ya Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho Ndaki ya Afya na Sayansi Shiriki (MCHAS).
Amesema, shabaha yao nikuongeza nguvu ya wataalamu nchini, hivyo watendaji wanawajibu wa kusimamia kiwango cha elimu kinachotolewa hakishuki na kamwe hatapenda kuona watu wa bora liende wakikiendesha chuo hicho.
“Sipendi kuona sifa hii ya elimu bora ikishukia Mbeya, sipendi kuwaona watu wanaosema bora liende tu, madaktari ni watu muhimu sana kwani wanashindana na uhai wa mtu usiondoke, hivyo sitaki kuona mchezo ukifanyika,”alisema.
Aidha, akijibu agizo hilo Naibu Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bonaventure Rutinwa, amesema kamwe hatakubali mtumishi au mwanafunzi yoyote kuharibu sifa ya chuo chuo hicho ambacho kimebahatika kutoa viongozi wakubwa watano wa Afrika.
“Chuo hiki kimewatoa viongozi wakubwa akiwemo Rais Magufuri, Rais wa Uganda Yower Kaguta Museven, Rais wa sasa wa Malawi, Bingu wa Mutarika, Rais Mstaafu wa Tazania awamu ya nne, Jakaya Kikwete, Rais wa awamu ya tatu Tanzania, Benjamin Mkapa na Rais wa zamani wa Sudan Kusini Dr. John Mabior,”alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments: