Mwenyekiti wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasa) Gen. Mstaafu Davis Mwamunyange ametembelea kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake katika Ofisi za Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco) kwa lengo la kujitambulisha na kufahamu majukumu ya shirika hilo.

Aidha ameipongeza menejimenti ya Shirika hilo kwa jitihada na mipango mizuri waliojiwekea katika kuboresha huduma ya Majisafi na Majitaka kufikia mwaka 2020 katika jiji la Dar es salaam na Miji ya Bagamoyo na Kibaha Mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kulia) akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja (Kushoto) wakati alipotembelea makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo katika eneo la Gerezani jijini Dar es Salaam akiwa na lengo la kujitambulisha na kufahamu majukumu ya shirika hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa ufafanuzi wa majukumu na utendaji kazi wa Shirika hilo kwa Mwenyekiti wa Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage katika kikao cha Menejimenti wakati alipokwenda kujitambulisha na kufahamu majukumu ya Shirika hilo ,jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: