Na Dokta Mathew.

Kitendo hiki ni pale mwanamke anapoweka uume wa mwenza wake mdomoni mwake na kuanza kunyonya kama pipi au mwanaume kuingiza ulimi ukeni pamoja na kunyonya via vya mwanamke pindi wapenzi hawa wawapo faragha.

Kumekua na ongezeko la kitendo hiki kwa vijana na imekua kama ni sehemu ya mahaba kwa wapenzi hata inafikia hatua mwanaume ANAONA MKE/MPENZI WAKE HAJUI MAHABA KAMA HAJAMNYONYA UUME AU MWANAMKE KUONA HIVYO ASIPONYONYWA YEYE.VILE VILE KUNA WANAWAKE WANAONA KUFANYA MAPENZI BILA KUNYONYA NI USHAMBA.

Vyumbani mambo mengi sana hutokea katika suala zima la mapenzi, nitaenda kusema kwa ufupi madhara ya kunyonya.

KISONONO CHA KOO.

Kama unafanya hiki kitendo halafu ukute mwanamke/mwanaume ana magonjwa ya zinaa kama kisonono inakua rahisi kwa mnyonyaji kuambukizwa. Kumbukeni kama mwanamke ana kisonono sio rahisi kumgundua kama ilivyo kwa mwanaume. TUWENI MAKINI.

SARATANI YA KOO.

Hii hasa huwapata wanawake ambao hupenda kunyonya uume wanaume wengi na hivyo kuwaweka katika hatari ya kuambukiwa vimelea wanaosababisha saratani hiyo mfano HPV.

KUBADILISHANA VIJIDUDU (BACTERIA).

Kama wote tunavofahamu ya kwamba kwenye miili yetu kuna vijidudu (bacteria) Rafiki (normal flora); sasa hao bacteria wakiingia sehemu ambayo sio yake huleta madhara kwani wameingia eneo ambalo hawajazoea, wataingia sehemu mpya kwa kuwanyonya kutoka kwa mwanamke au mwanaume. Hii inaweza isilete madhara mapema lakini uendeleaji wa kunyonya nyonya wanaume au wanawake wengi mara kwa mara hupelekea kupata madhara mengi na mengine ni magumu kutibu.

Kupata Maambukizi ya HIV.

Kupata madonda mdomoni.

Kujiweka katika hatari ya kupata saratani za mdomo, ulimi nk.

SASA WADAU WANGU MPAKA HAPO NIMEFIKIA MWISHO WA MAKALA FUPI. TUJIHADHARI NA VITENDO HATARISHI AMBAVYO TUMEIGA KUTOKA KWA WAZUNGU. SOTE TUNAFAHAMU KAZI YA MDOMO NA ULIMI KWA HIYO TUSIVIFANYIE KAZI AMBAYO SIO YAKE ACHENI KUSHABIKIA PAGE, MAKUNDI YA WATSAP, VIDEO AMBAZO ZINAHAMASISHA UFANYAJI WA HAYA MAMBO. ZIPUUENI KWANI HAO WANAOHAMASISHA WENGI WAO NI WAFANYABIASHARA WA NGONO NA HAWAWATAKII MEMA WATU WEMA.

Kwa dondoo zaidi za Afya hebu follow page yake ya instagram kwa jina @doktamathew
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

5 comments: