Rais wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga, akiimba wakati wa ibada iliyofanyika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Anglikana Jijini Dodoma leo.
Watoto kutoka Kanisa la Anglikana Msalato wakiimba katika ibada hiyo.
Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Jijini Dar es Salaam, Madamu Ruth Mwamfupe akiimba katika ibada hiyo huku akisindikizwa na waumini wa kanisa hilo.
Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
Waumini wakiwa ibadani.
Kwaya ya watoto kutoka Msalato ikitoa burudani ya nyimbo za injili.
Mwanamuziki Mzee Makasy ambaye hivi sasa ni mwimbaji wa nyimbo za injili baada ya kuokoka akitoa burudani.
Raia wa kigeni ambao wanasali katika kanisa hilo wakifurahi matukio mbalimbali ya uimbaji.
Mwimbaji wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha kutoka Dar es Salaam, akiimba.
Katibu wa TAMUFO ambaye pia ni Muimbaji wa nyimbo za injili Stellah Joel, akiimba.
Viongozi wa dini wa kanisa hilo wakisalimiana na Emmanuel Mbasha ambaye ni muimbaji wa nyimbo za injili.
Na Dotto Mwaibale, Dodoma.
WAIMBAJI wa Nyimbo za injili ambao ni wanachama wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO), leo wameshiriki ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Anglikana Jijini Dodoma ambapo pia walipata fursa ya kutoa burudani ya nyimbo mbalimbali ikiwa ni njia ya kuhubiri na kulifanya kanisa hilo kuwaka moto wa furaha kutokana na burudani safi kutoka kwa watumishi hao wa mungu.
Wanamziki hao ambao wapo jijini Dodoma wamepokelewa na Kanisa hilo na kesho watatembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia umoja wao TAMUFO.
Mbali ya kesho kwenda Bungeni leo jioni watashiriki katika tamasha kubwa la nyimbo za injili ambalo litaenda sanjari na uzinduzi wa Albam ya nyimbo ya injili ya Kwaya ya Safina ambayo ipo katika hilo Kuu la Anglikana Dodoma ambapo kwaya mbalimbali zitatoa burudani ya nyimbo za kuabudu.
Akizungumzia kuhusu wanamuziki hao Rais wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga, alisema wanayofuraha ya kufika Dodoma salama na kuwa leo hii watashiriki katika tamasha hilo na kesho asubuhi watakwenda kutembelea Bunge.
Katibu wa TAMUFO, Stellah Joel, amesema makundi mbalimbali ya wanamuziki wanaounda umoja huo yatakuwepo kama vile, waimbaji wa nyimbo za injili, Dansi, Bongo Fleva, Muziki wa Asili na Taarabu.
"Wanamuzi wote kutoka katika makundi hayo tayari wamefika Dodoma na kuwa maandalizi yote yamekamilika.
Amewataja baadhi ya wanamuziki hao kuwa ni Hamza Kalala, Mzee Makasy, Witness Mweupe, Emanuel Mbasha, Madamu Ruth Mwamfupe , Happyness Sanga kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na wengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments: