Mjumbe wa halmashauri kuu (MNEC UWT), Halima Okashi akitoa zawadi kwa Mmoja ya Wanawake waliolazw aktika wodi ya wamama katika Hospitali ya Mwananyamala ambapo UWT Kinondoni walifika katika hospitali hiyo kutoa Msaada katika kuadhimisha siku ya Wanawake Dunia.
Katibu wa UWT CCM Wilaya ya Kinondoni, Nuru Mwaibako, akiwa na Diwani Viti maalum CCM Kinondoni Frolenece Masunga wakikabidhi zawadi kwa Wanawake waliofka katika Clinic ya Hospitali ya Mwananyamala na watoto wao, UWT Kinondoni wamefanya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatembelea wamama waliopo katika Hospitali ya Mwananyamala.
Diwani Viti maalum CCM Kinondoni Frolenece Masunga akiwa amemshika mmoja ya Watoto waliofika kutibiwa katika Hospitali ya Mwananyamala leo wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.
Ujumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni kwa Pamoja wakimkabidhi zawadi Mganga wa Hospitlai hiyo kwa ajili ya Wanawake wa Hospitali hiyo.
Ujumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni, ukiwasili katika Hospitali ya Mwananyamala ukiongozwa na Mjumbe wa halmashauri kuu (MNEC UWT), Halima Okashi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: