Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua semina ya wanawake wa Manispaa ya Shinyanga iliyoandaliwa na SHUWASA kama moja ya matukio ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Akina mama wa Manispaa ya Shinyanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA), Injinia Sylivester Mahole akiwasisitiza akina mama kuendelea kushirikiana na SHUWASA katika kutatua changamoto zinazojitokeza katika utoaji huduma za maji safi na usafi wa mazingira.
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Joyce Egina akizungumza wakati wa semina hiyo.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa ukumbini: Wa kwanza kushoto ni Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard ,katikati ni Afisa TEHAMA SHUWASA,Amosi Stephen akifuatiwa na Meneja Utawala na Rasilimali Watu SHUWASA, Flaviana Kifizi.
Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akitoa mada kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja. Aliwataka wateja kutoruhusu vitendo vya rushwa katika huduma za maji na kuwataka wateja kutunza mita za maji na kuhakikisha wanalipa ankara za maji kwa wakati.
Afisa TEHAMA wa SHUWASA, Amosi Stephen akielezea jinsi walivyoboresha huduma za ulipaji wa ankara za maji ambapo hivi wateja sasa wanafurahia huduma na kutumia simu na benki kulipa ankara za maji.
Mwenyekiti wa semina hiyo, Ziphora Pangani (Mkuu wa wilaya mstaafu) akiongoza kipindi cha majadiliano wakati wa semina.
Mwinjilisti Esther Emmanuel akichangia hoja ukumbini.
Bora Yusuph akizungumza wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo,Diana Ezekiel
Joyce Masunga (mbunge mstaafu) akichangia hoja wakati wa semina hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na akina mama wakicheza muziki/wimbo wa Wanawake na Maendeleo. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: