Mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup, Shafii Dauda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya michuano ya Ndondo Cup itayoanza kutifuana Mwezi ujao mwaka huu leo katika fukwe za Escape 1 Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Na Agness Francis, Globu ya jamii.
Mashindano ya Ndondo Cup mwaka 2018 yamezinduliwa leo rasmi, ambayo yanafanyika kwa msimu wa 5 mwaka huu ambapo msimu huu yatafanyika katika mikoa mita5 u Ambayo ni Dar es Salam, Mwanza na Ruvuma.
Mkoa wa Dar es Salaam utafungua mashindano hayo tarehe 6 mwezi wa 4 mpaka 6 mwezi wa 5 mwaka huu na baada ya kupatikana kwa Timu 32 kutoka kwenye hatua za awali yatapangwa rasmi makundi kwa Timu zitakazoshiriki zitaanza kumenyana katika Uwanja wa Bandari na Kinesi kuanzia tarehe 1 mwezi wa 6 mpaka 22 mwezi wa 7 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja vya Escape 1 Mikocheni Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa maandalizi ya mashindano hayo Shafii Dauda amesema kuwa zoezi la usajili katika mkoa wa Dar es salaam litaanza leo kupitia usimamizi wa chama cha soka mkoa (DRFA) ambapo Ada ya usajili ni shilingi laki 3 zitakazo lipwa kupitia akaunti ya chama hicho.
Dauda ameongezea kuwa kwa mshindi wa kwanza kwa Dar es salaam atapata zawadi ya shilingi milioni 10,mshindi wa pili milioni 5,mshindi wa 3 atapata milioni 3 na mshindi wa nne milioni 1.
"Mbali na zawadi hizi za mshindi wa kwanza hadi wa nne Timu zote zitakazoingia kwenye hatua ya 16 bora zitapewa kiasi cha laki 5 kwakila Timu kwaajili ya maandalizi na pia zitakuwa zikipewa usafiri wa kuwachukua kuwapelekea Uwanjani na kuwarudisha majumbani kwakila siku ya mechi pamoja na Chakula, na kwaTimu zitakazo ingia 8 bora zitapewa kiasi cha shilingi milioni 1 kwakila Timu kwaajili ya maandalizi pia kwa Timu zitakazo ingia 4 bora zitapewa kiasi cha shilingi milioni 1.5 za maandalizi kwa kila Timu na kwahatua ya mwisho Ambayo ni fainali kila Timu itapewa kiasi cha shilingi milioni 2 za maandalizi" amesema Dauda.
Toa Maoni Yako:
0 comments: