1. Usimuumize moyo wake kwa namna yeyote ile.

2. Usi 'pretend' unampenda ili ufanikiwe kufanya jambo fulani kama vile kulala nae.

3. Mtukane vyo vyote vile ila sio wazazi wake na kumwambia kuwa yeye ni mbaya.

4. Usimfananishe na wanawake zako amabao ulisha wahi kutembea nao.

5. Usimchukulie kirahisi rahisi (Never take her love for granted) yaani wakawaida.

6. Usimpige

7. Usimsaliti na kuonyesha kabisa dharau ajue kuwa una 'cheat'

8. Usimvunjie heshima kwa kumgombeza mbele za watu.

9. Usimpotezee muda wake kama hauna mpango wa kumuoa maana unamchelewesha kupata mume bora.

10. Usimfanye ajione hapendwi na ana mkosi hapa ulimwenguni.

11. Usimbake

12. Kamwe usisahau kumwambia unampenda na yeye ni mzuri.

13. Usimpe mimba na kumkimbia au kumwambia aitoe, kama huna nia ya kumuoa achana na hayo mambo, nadhani unajua kabisa matokeo ya kufanya ngono.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: