Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (Kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidi wa Uchaguzi Katika Manispaa ya Moshi 20.11.2017. Kushoto ni Mwanasheria Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Mtibora Selemani.

Na Clarence Nanyaro – NEC, MOSHI

Mwenyekeiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage amewataka wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi nchini Kuwashirikisha Viongozi wa Vyama vya siasa katika maamuzi mbalimbali wanayofanya yenye maslahi kwa pande zote ili kuendeleza amani na utulivu ulipo nchini.

Akizungumza na Wasimamizi wa uchaguzi katika Manispaa ya Moshi, Jaji Kaijage alisema kuwa katika kipindi hiki ambapo vyama vinashiriki katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakafanyika Novemba 26,2017 ni muhimu kwa Wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kuwa Maadili ya Uchaguzi wakati wa kampeni yanazingatiwa ili kuepusha uvunjifu wa amani miongoni mwa wananchi.

Jaji Kaijage ambaye yuko katika ziara ya kutembelea Mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha kushuhudia utekelezaji wa maadili ya Uchaguzi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani, amewataka Wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kuwa Vifaa vyote ambavyo vinahitajika ili uchaguzi uweze kufanyika vimepatikana na vile ambavyo havijapatika wawasiliane na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kasoro zinazobainika ziweze kupatiwa ufumbuzi mapema kabla ya siku ya Uchaguzi.

Wakati katika mkoa wa Tanga Uchaguzi utafanyika Katika Kata ya Majengo iliyoko katika Halmshauri ya Mji Korogwe,Mkoani Kilimanjaro,Uchaguzi mdogo wa Udiwani utafanyika katika Kata ya Bomambuzi katika Manispaa ya Moshi na Katika Kata za Machame Magharibi ,WeruWeru na Mnadani katika Halmashauri ya Hai.

Aidha,Jaji Kaijage alitoa wito kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kuhakikisha Kuwa siku ya Upigaji Kura ulinzi unaimarishwa katika Vituo vya Kupigia kura lakini usiwe ulinzi wa kuwatia wananchi hofu wakashindwa kufika katika vituo vya kupigia kura viongozi wanaowataka ili washirikiane nao katika kujiletea Maendeleo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: