Ng'ombe, akishatoa maziwa ya kulisha familia nzima, hurejea katika malisho yake taratibu. Lakini kuku, akishataga yai moja hupiga kelele ili kila mtu ajue. Je! Yai hilo alilotaga laweza kutosha hata kwa mlo wa mtu mmoja? Jibu ni hapana.

Katika maisha kuna watu wa aina 2 kuna wale wanaofanana na Ng'ombe na wale wanaofanana na Kuku.

Mtu afananaye na kuku akikusaidia jambo hata kama ni dogo sana atasema kila mahali ili watu wote wajue jambo hilo. Kama ni kazini/msikitini atahakikisha anajisifu sana na kuisambaza ile habari kwa wengi. Kuna watu walisaidiwa na watu hawa wenye tabia ya kuku baadaye wakaishia kuumizwa mioyo yao baada ya kusambaa kwa habari hiyo.

Mtu mwenye tabia ya kuku akitoa msaada hata kwenye kituo cha watoto yatima, au akisaidia maskini anatamani aje na waandishi wa habari.

Kuna watu wenye tabia ya ng'ombe. Akikusaidia hata kama ni jambo kubwa sana kiasi cha kushindwa kumlipa fadhila, hawezi kukusema na hataki watu wajue. Furaha yake ni kukuona unavuka salama na unafanikiwa. Watu wa namna hii hupata thawabu kubwa. Tamani kuwa na tabia kama hii ya kusaidia bila kujitafutia utukufu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: