Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo. Kushoto ni Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo. Kushoto ni Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo.Kulia ni Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh.

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania, leo imetangaza dili za kipekee zinazohusu simu za Smartphone ambazo zitahakikisha kila mtu anakuwa sehemu ya maisha ya kidigitali katika msimu huu wa Krismasi na mwaka mpya.

Akitangaza ofa hizo za msimu wa sikukuu Dar es Salaam leo, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema dili hizo kemkem zinapatikana kwa kupiga namba ya menu mpya *147*00# na kubonyeza kitufe cha ‘Duka la Simu’ ili kuchagua simu unayoipenda, na kisha kutembelea Duka lolote la Tigo nchi nzima ili kuchukua simu uliyoichagua.

‘Katika ofa ya kwanza, wateja wa Tigo wanaweza kupata simu ya Smartphone BURE kirahisi kwa kununua bando kuanzia TZS 25 000 ambayo - pamoja na Smartphone ya bure – inawapa 1GB data, SMS 50 na dakika 50 za kupiga Tigo – Tigo,’ alisema.

Katika dili ya pili, wateja wa Tigo pia wanaweza kupata Smartphone kwa kuchagua mpango wa kulipia kwa miezi sita. Ofa hii inawahusu wateja wa sasa wa Tigo ambao wanakidhi vigezo vilivyowekwa.

Katika msimu huu wa sikukuu, Tigo pia inatoa ofa ya ‘Lipia sasa, Chukua Baadaye’ nambapo wateja wanaruhusiwa kuchagua simu yoyote ile wanayoipenda na kisha kufanya malipo ya awamu kila mwezi, ambapo wataruhusiwa kuchukua simu waliyoichagua baada ya kumaliza mpango wa malipo ya kila mwezi.

‘Kupitia ofa hizi kabambe, Tigo inaendelea kushika hatamu za ubunifu unaoendana na mahitaji ya wateja kwa kuwezesha kila mtu kumiliki mojawapo ya hizi simu bomba za Smartphone, ambazo zimeunganisha na mitandao ya jamii. Hii ndio njia yetu ya kuhakikisha kuwa kila mtu anakuwa sehemu ya maisha na mabadiliko ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo,’ David alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: