Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza leo Novemba 21, 2017 kuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe amejiuzulu. Spika Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha reuters.

Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano.

Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii. Amekuwa mamlakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980.Bwana Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: